DRC na Rwanda zakubaliana kuhusu mpango wa kulidhibiti kundi la waasi wa FDLR

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Nchi za DRC na Rwanda, zimekubaliana kuhusu mpango wa kudhibiti na kulitokomeza kundi la FDLR,ambalo Rwanda imekuwa ikidai kwamba DRC inalifadhilii

Makundi yenye silaha ikiwemo M23 na FDLR yamekuwa yakitatiza usalama wa raia mashariki ya DRC.
Makundi yenye silaha ikiwemo M23 na FDLR yamekuwa yakitatiza usalama wa raia mashariki ya DRC. © Alexis Huguet / AFP

Ni makubaliano ambayo yameafikiwa kufutia mkutano wa mataifa hayo mawili chini ya mpatanishi wake taifa la Angola, mkutano uliofanyika mwishoni mwa juma.

Jukumu hilo sasa limeachiwa wataalamu ambao watabuni mikakati ya kutekeleza mpango wa kulidhibiti na kulinyanganya silaha kundi la FDLR ambalo, linadaiwa kuendeleza shughuli zake mashariki wa DRC, ripoti ya wataalamu hao ikitarajiwa kujadiliwa kabla ya kuidhinishwa na mataifa husika.

Mkutano huo uliowaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje kutoka RwandaDRC na Angola pia wamekubaliana kutekeleza rasimu ya mapendekezo ya kupatika kwa amani mashariki mwa DRC.

Rwanda ambayo wanajeshi wake wanadaiwa kuunga mkono waasi wa M23 mashariki mwa DRC, imesema itaondoka DRC iwapo kundi la FDLR litakandamizwa, kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa diplomasia kutoka DRC katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Kwa muda sasa DRC na Rwanda zimekuwa katika mazungumzo chini ya mpatanishi taifa la Angola ili kujaribu kupata suluhu la kudumu kwa utovu wa usalama mashariki mwa DRC.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment