Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi hivi karibuni siku ya Jumamosi Oktoba 12 alitangaza kuendelea kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya jeshi la Kongo na jeshi la Uganda katika mapambano dhidi ya waasi wa ADF katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Uamuzi huo ulithibitishwa baada ya mkutano wa kutathmini operesheni katika mji mkuu wa Kongo kuanzia Oktoba 10 hadi 11, 2024 kati ya wakuu wa majeshi ya Kongo na Uganda.

Kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Kongo, kwenye akaunti yake ya X (zamani ikiitwa Twitter), mkuu huyo wa nchi alitoa maelekezo ya wazi ya kuimarishwa kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya DRC na Uganda ili kutokomeza ukosefu wa usalama katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.
Tangazo la kuendelea kwa ushirikiano huu wa kijeshi linakuja huku Uganda ikilaumiwa na mashirika ya kiraia kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.
Operesheni za pamoja
Operesheni za pamoja kati ya jeshi la Kongo na jeshi la Uganda zilianzishwa mnamo Novemba 30, 2021 dhidi ya ADF, washirika wa Islamic State, wanaoshutumiwa kuhusika katika mauaji ya mamia ya raia katika mikoa hii.
Kwa mujibu wa majeshi hayo mawili, mafanikio na maendeleo kadhaa yamebainishwa katika ardhi hiyo. Kanali Mak Hazukay, msemaji wa operesheni za UPDF na FARDC, alisema kuwa wapiganaji 52 wa Allied Democratic Forces waliuawa na wengine 72 walikamatwa kati ya mwezi wa Aprili na Septemba 2024.
Ufafanuzi wa mahusiano ya kidiplomasia
Mnamo Agosti 2024, mashirika ya kiraia katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kusini yaliiomba serikali ya Kongo kufafanua uhusiano wa kidiplomasia na Uganda, ambayo pia inawaunga mkono waasi wa M23, wanaoungwa mkono pia na Rwanda.
Ripoti ya hivi punde kutoka kwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa inashutumu Uganda kwa kuowezesha mikutano ya maafisa wa M23-AFC nchini Uganda. Washirika wa karibu wa Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kamanda wa vikosi vya Uganda, walinyooshewa kidole katika ripoti hii. Jenerali Muhoozi Kainerugaba, katika taarifa zake kwenye ukurasa wake wa X, hafichi kuuga mkono M23.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.