China yaanzisha mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa na Taiwan

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

China imeanzisha mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa cha Tiawan, wizara ya ulinzi ya China ikisema ni onya kwa vikosi vya Taiwan.

Meli ya usambazaji ya Ufilipino (katikati) ikijaribu kukwepa mojawapo ya meli za walinzi wa baharini wa China iliyojaribu kuiizuia katika eneo la Thomas Shoal, Ayungin Shoal, kwenye eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya China Jumanne, Aug. 22, 2023.
Meli ya usambazaji ya Ufilipino (katikati) ikijaribu kukwepa mojawapo ya meli za walinzi wa baharini wa China iliyojaribu kuiizuia katika eneo la Thomas Shoal, Ayungin Shoal, kwenye eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya China Jumanne, Aug. 22, 2023. AP – Aaron Favila

Mazoezi hayo ya kijishi yaliopewa jina Sword-2024B, yanafanyia majaribio uwezo wa vikosi vya ndani vya China, Beijing ikisema mazoezi hayo yatafanyika eneo la Kaskazini na mashariki mwa kisiwa cha Taiwan bila kutoa taarifa ni lini mazoezi hayo yatakamilika.

Taiwan kwa upande mwingine imesema imetuma vikosi vyake kukabiliana na uvamizi wowote wa China.

China imekuwa ikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho huru cha Taiwan, ambacho imesisitiza kuwa ni sehemu ya himaya yake, kwa kutuma ndege za kijeshi pamoja na meli.

Hata hivyo China haijawahi weka wazi iwapo inaweza au la kutumia nguvu kuchukuwa udhibiti wa kisiwa cha Taiwan.

Marekani mshirika wa karibu wa Taiwan, ameonya China dhidi ya kuvamia Taiwan

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment