Daktari aliyepandikiza korodani za mbuzi kwa wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

John Romulus

Usiku mmoja mwaka wa 1917, mkulima mmoja, aliyehangaikia hamu yake ya mapenzi, alimtembelea daktari katika mji mdogo huko Kansas, Marekani.

‘Hakuweza kusimama’ kwa muda mrefu, alisema: “Ni kama tairi la lililopasuka.”

“Nimeenda kwa madaktari wengi na kutumia pesa nyingi, na hakuna hata mmoja wao aliyenisaidia chochote.”

“Nimekuwa na kesi nyingi kama zako,” daktari alijibu. “Nimetumia seramu, dawa na umeme kwa wanaume wenye tatizo hilo. Sidhani kama nimewahi kumnufaisha mgonjwa yeyote kati yao.”

“Sayansi ya matibabu haijui chochote ambacho kinaweza kusaidia na hali kama yako,” alisema.

Alipchungulia dirishani, akaona mbuzi na kusema: “Hungekuwa na shida kama ungekuwa mbuzi.”

“Ningekuwa na korodani za mbuzi? Nipe!” alisema mkulima.

“Zinaweza kukuua,” daktari alionya.

“Lakini ni hatari inayofaa ,” lilikuwa jibu la mkulima.

Hili ni toleo la mazungumzo.

Kuna mengine, yalio na maelezo zaidi, kadhaa ambayo ni ngumu kudhibitisha kwani hii ni hadithi yenye vidokezo.

Lakini ingawa inaweza kuonekana kuwa ya kushangaza kwako, ni kisa cha kweli.

Na inasimuliwa si kwa sababu tu ni ya kipekee bali pia kwa sababu inaonyesha jinsi watu wanavyoweza kuwa na hamu ya kupata tiba, na jinsi ilivyo vigumu kuwadhibiti waganga.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment