Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya Afrika Leo Jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja.
Muhtasari
- Serikali ya Uingereza ‘imetiwa hofu sana’ na mashambulizi ya Israel dhidi ya kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon
- Mguu wa mpanda milima aliyetoweka miaka 100 wapatikana
- Zelensky akutana na Papa Vatican
- Rais wa Kenya atoa mwito wa fedha za dharura kwa ajili ya ujumbe wa Haiti
- Shambulizi la Beirut: Wafanyakazi wa uokoaji watafuta dalili za waliopotea chini ya vifusi
- Tazama: Uharibifu mkubwa uliosababishwa na Kimbunga Milton Florida Marekani
- Mashambulizi ya Israel Beirut: Je, mkakati wa Israeli ni upi, na wanajaribu kufikia nini?
- Jaji Mkuu Kenya kuunda jopo la majaji wa kusikiza kesi ya kupinga kuondolewa madarakani kwa Gachagua
- Mwanamke wa Australia ang’atwa mkono katika shambulio la mbwa
- Watu wenye silaha wamewaua wachimba migodi 20 nchini Pakistan
- Obama ahimiza wapiga kura kumuunga mkono Harris katika kinyang’anyiro ‘kikali’ cha urais
- Kampuni zinazohusishwa na Uingereza zashukiwa kukiuka vikwazo dhidi ya Urusi
- Eritrea, Misri na Somalia ‘zaboresha ushirikiano dhidi ya Ethiopia’
- Kimbunga Milton: Idadi ya vifo yafikia 16
- Umoja wa Mataifa waishutumu Israel kwa uhalifu wa kivita kutokana na mashambulizi dhidi ya hospitali za Gaza
- Watu 22 wameuawa katika mashambulizi ya Israel huko Beirut – Lebanon
- Serikali ya Uingereza ‘imetiwa hofu sana’ na mashambulizi ya Israel dhidi ya kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon
Chanzo cha picha,PA MediaMsemaji wa Downing Street amesema serikali “imetiwa hofu sana” na ripoti kwamba Israel imefyatua risasi kwa makusudi katika kituo cha uchunguzi kinachomilikiwa na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon.Hii inafuatia taarifa kutoka kwa kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon ambacho kimesema kuwa kifaru cha jeshi la Israel kilishambulia vituo vya shirika la Umoja wa Mataifa (Unifil) kusini mwa Lebanon jana, na kushambulia mnara wa uchunguzi wa umoja huo na kuwajeruhi walinda amani wawili.Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kila siku wa Downing Street, msemaji huyo alisema: “Tulishangaa kusikia taarifa hizo na ni muhimu kwa walinda amani na raia kulindwa.”Kama mnavyofahamu, tunaendelea kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na kumalizika kwa mateso na umwagaji damu. Ni ukumbusho wa umuhimu wa sisi sote kufanya upya juhudi zetu za kidiplomasia kutatua hili.”Alipoulizwa ikiwa waziri mkuu atakubaliana na wazir mkuu wa Ireland kwamba Israeli imevunja sheria ya kimataifa, msemaji huyo anasema: “pande zote lazima zifanye kila linalowezekana kuwalinda raia na kuzingatia sheria za kimataifa.Mshirikishe mwenzako, Serikali ya Uingereza ‘imetiwa hofu sana’ na mashambulizi ya Israel dhidi ya kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon - Mguu wa mpanda milima aliyetoweka miaka 100 wapatikana
Chanzo cha picha,Jimmy ChinMguu unaoaminika kuwa wa mpanda mlima wa Uingereza aliyetoweka miaka 100 iliyopita umepatikana kwenye Mlima Everest, katika ugunduzi ambao unaweza kutatua moja ya siri kubwa za wapanda milima.Andrew Comyn “Sandy” Irvine alijaribu kupanda Mlima Everest mnamo mwezi Juni 1924 na mshiriki mwenzake George Mallory wakati wawili hao walipotoweka.Huku mabaki ya mwili wa George hatimaye yalipatikana, mwili wa Irvine haukugunduliwa kamwe.Lakini mwezi uliopita timu ya wapanda mlima walipokuwa wakirekodi filamu ya National Geographic waligundua mguu uliokuwa umejificha kwenye barafu inayoyeyuka.
Chanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Sandy Irvine, kama alivyojulikana sana, alikuwa na umri wa miaka 22 alipotoweka,Mpandamlima huyo mashuhuri Jimmy Chin, ambaye aliongoza timu, alisifu ugunduzi huo kama “wakati wa kumbukumbu na wa hisia”.Kwa miaka mingi, watu wengi wamejaribu kuutafuta mwili wa Irvine kwani inasemekana alikuwa amebeba kamera yenye filamu ambayo haijatengenezwa ambayo inaweza kuthibitisha kuwa yeye na mwenzake George Mallory walifanikiwa kufika kwenye kilele cha mlima.Familia sasa imetoa sampuli ya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa ni Irvine – lakini timu ya watengenezaji filamu ina uhakika kuwa ni mali ya Irvine, kutokana na soksi iliyopatikana ndani ya buti hiyo kupambwa kwa maneno “AC Irvine”.Mshirikishe mwenzako, Mguu wa mpanda milima aliyetoweka miaka 100 wapatikana Zelensky akutana na Papa Vatican
Chanzo cha picha,Getty ImagesRais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekutana na Papa Francis mjini Vatican.Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mkutano wao katika jumba la kitume la Vatican ilidumu kwa dakika 35.Huu ni mkutano wa pili kati ya Zelensky na Papa Francis katika kipindi cha miezi michache iliyopita, shirika hilo linasema.
Chanzo cha picha,Getty ImagesKulingana na shirika la habari la ANSA , Papa Francis alimkabidhi Zelensky shada ya maua yenye maandishi “Amani ni maua dhaifu.”Rais wa Ukraine alimkabidhi papa huyo mchoro wa mafuta, “Mauaji ya Bucha. Hadithi ya Marichka,” ambayo inaonyesha msichana akiwa katikati ya magofu katika mji wa Bucha uliopo karibu na Kiev.
Uganda yafuta leseni ya kampuni ya Uchina ya kuchimba madini

Mgodi wa Kilembe iko katika wilaya ya Kasese katika eneo la Magharibi mwa Uganda. / Picha: Reuters
Mgodi wa Kilembe iko katika wilaya ya Kasese katika eneo la Magharibi mwa Uganda. / Picha: Reuters
Waziri wa Nchi anayeshughulikia uwekezaji nchini Uganda, Evelyn Anite, alitangaza kwamba Uganda imesimamisha mkataba wake na Tibet-Hima, mfanyabiashara wa Mgodi wa Kilembe wa kutoka Uchina.
Mgodi wa Kilembe uko katika Wilaya ya Kasese katika eneo la magharibi mwa Uganda.
Waziri Anite alisema hii baada ya mwekezaji huyo kutaka kusafirisha tani 30,000 za dhahabu, shaba na kobalti kama sampuli kwa ajili ya majaribio nchini China.
Anite aliyasema hayo alipofika mbele ya Kamati ya Bunge ya Maliasili, ambapo aliitwa kueleza hatua iliyofikiwa ya ufufuaji wa Migodi ya Kilembe Wilayani Kasese.
“Mkandarasi huyu alitaka serikali imruhusu kuchukua tani 30,000 za shaba, kobalti na dhahabu kwa ajili ya sampuli tu. Haikuwa busara kwa mwanakandarasi kufikiria kwamba tungeruhusu kiasi kikubwa kama hicho cha maliasili kuondoka nchini,” Anite alieleza.
Alieleza sababu kuu za kusitishwa kwa mkataba huo .
Kwanza wingi wa bidhaa ambazo mwekezaji alitafuta kwa ajili ya majaribio, pili madai kuwa mgodi ulijaa maji, na tatu baadaye ugunduzi wa uzembe wa mwekezaji kusimamia operesheni hiyo kubwa.
“Rais ( Yoweri Museveni) alisema kuwa rasilimali hizi ni za Wananchi wa Uganda. Tibet-Hima walipogundua hilo, walionyesha kwamba hawataendeleza mkataba huo, kama ilivyobainishwa katika ripoti ya tume. Ilikuwa ni jambo lisilokubalika kwa Rais, kwangu na kwa Serikali kwa ujumla,” alisema Anite.
Mamalamiko ya kampuni ya Tibet-Hima
Uchunguzi wa Bunge kuhusu kandarasi hiyo ya uchimbaji wa madini ulianzishwa kufuatia ombi la Solomon Silwany mbunge wa Bukooli ya Kati, Aprili 2024, lililoomba uchunguzi kuhusu mazingira ya kusitishwa kwa mkataba wa kampuni ya Tibet-Hima wa kusimamia, kukarabati na kuendesha Migodi ya Kilembe kwa miaka 25.
Kwa mujibu wa Silwany, Serikali ilishindwa kutimiza wajibu wake chini ya mkataba huo, hivyo kusababisha kampuni ya madini ya Tibet-Hima kupata hasara ya dola milioni 980 (shilingi trilioni 3.581) kati ya 2014 na 2017.
“Kampuni ilitoa shilingi bilioni 4.2 kwa serikali, ikaajiri wananchi 822 moja kwa moja, akanunua vifaa vya thamani ya dola milioni 22 (shilingi bilioni 80.411 ), na alitoa dola milioni 183.5 (shilingi bilioni 676.187) kwa uwekezaji wa siku zijazo katika kurejesha uzalishaji wa madini ya shaba kutoka kwa Kilembe, ” Silwany aliiambia Kamati ya Bunge.
Kampuni ya Tibet-Hima Ltd pia ilitaja malalamiko kadhaa dhidi ya Serikali ya Uganda, kuwa ni pamoja na kushindwa kukabidhi eneo la Mgodi wa Kilembe ndani ya miezi tisa baada ya kusainiwa kwa mkataba na uamuzi wa Serikali kupunguza muda wa mkataba kutoka miaka 25 hadi 15 na hivyo kusababisha kusitishwa kwa mkataba.
Waziri Anite alielezea kamati ya Bunge kuwa hajutii uamuzi wake wa kusitisha mkataba na Tibet-Hima.
Zanzibar yatafuta uwekezaji ili kuulinda Mji Mkongwe
Rais Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar amezitaka taasisi na wadau wengine kujitokeza kushirikiana na Serikali yake kuhifadhi maeneo ya urithi ikiwemo Mji Mkongwe kwani una majengo mengi yanayohitaji ukarabati na kutunzwa kwa fedha na utaalamuZanzibar inatafuta wadau na washirika zaidi katika juhudi zake za kuutunza na kuuhifadhi Mji Mkongwe / Picha:TRT AFRIKA
Zanzibar inatafuta wadau na washirika zaidi katika juhudi zake za kuutunza na kuuhifadhi Mji Mkongwe kutokana na umuhimu wake katika kuchangia pato la uchumi wa visiwa hivyo vya marashi ya karafuu.
Wito umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi siku ya Alhamisi 10 Oktoba, alipokutana Ikulu Zanzibar na ujumbe kutoka Taasisi ya “International National Trust Organization” ya Uingereza.
Wajumbe hao walimueleza mafanikio waliyoyapata katika kulifanyia ukarabati jengo la “Custom House” liliopo Forodhani maarufu jengo la Mizingani.

Mkutano huo uliosheheni wataalamu wa masuala ya uhifadhi wa miji ya urithi, ulihudhuriwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga, pia ulijumuisha taasisi za uhifadhi miji ya urithi kutoka Uingereza, Uganda, Jordan na Misri.
Rais Mwinyi amesema mbali na Mji Mkongwe kuwa katika eneo la Urithi wa dunia, lakini ni muhimu pia katika kukuza kukuza uchumi wa visiwa vya Zanzibar.

Kupitia Sekta ya Utalii, fedha nyingi za kigeni zinaingia serikalini kutokana na kuwa eneo linalotembelewa na wageni wengi.
Rais Mwinyi aliweka wazi furaha yake kwa juhudi na hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe (JUHIMKO) katika kufanya ukarabati mkubwa jengo la Mizingani.
Watu wajitokeze tuulinde Mji Mkongwe
Katika mazungumzo yake Rais Mwinyi, alizitaka taasisi na wadau wengine kujitokeza kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuhifadhi maeneo ya urithi ikiwemo Mji Mkongwe kwani una majengo mengi yanayohitaji ukarabati na kutunzwa kwa fedha na utaalamu.
Naye David Antony Simpson, Meneja Miradi wa Taasisi ya “International National Trust Organization”, akizungumzia changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, amesema kuongezeka kwa kina cha bahari ni miongoni mwa changamoto inayoikabili miji mingi ya urithi duniani iliyoko pembezoni mwa bahari kama ilivyo kwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Simson, ameahidi kuwa taasisi yake itaendeleza ushirikiano na Zanzibar ili kuhakikisha Mji Mkongwe unabaki kwenye ramani ya dunia.
Taasisi hiyo yenye uzoefu kwa nchi 102 duniani wa kufanya ukarabati wa miji mikongwe, takriban paundi 80,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi milioni 280 zilitumika kulifanyia ukarabati jengo la Mizingani chini ya ufadhili wa Mfuko wa Baraza la Urithi la Uingereza
Kenya yaahidi kupeleka maafisa wengine 600 wa polisi nchini Haiti
Rais wa Kenya William Ruto ametangaza siku ya Ijumaa Oktoba 11, 2024 kwamba maafisa 600 wa ziada wa polisi watatumwa kwa misheni ya kimataifa ya usaidizi wa usalama nchini Haiti, wakati Waziri Mkuu wa nchi hii iliyoharibiwa na vita vya magenge alipokuwa ziarani nchini Kenya.

Kenya ilianza kupeleka wanajeshi wake wa kwanza nchini Haiti msimu huu wa joto, ambao sasa wana idadi ya chini ya maafisa wa polisi 400, pamoja na takriban maafisa zaidi ya ishirini wa polisi kutoka Jamaica na Belize.
“Ninafuraha kutangaza kwamba maafisa wengine 600 wa polisi wa Kenya wanamaliza mafunzo yao kabla ya kutumwa na watakuwa tayari kuanza majukumu yao mwezi ujao,” Ruto amesema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Haiti, Garry.
Bw Ruto, ambaye alitoa hakikisho mwishoni mwa mwezi wa Septemba kwamba nchi yake itakamilisha kutumwa kwa maafisa 2,500 wa polisi kufikia mwezi Januari 2025, hakubainisha ni lini maafisa hao 600 wa ziada wa polisi watatumwa. Rais wa Kenya pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa “haraka” kuunga mkono misheni hii ambayo inakabiliwa na ukosefu wa fedha na vifaa.
“Tungependa kuona jibu la haraka, tungependa kuona kujitolea zaidi na tutaendelea kuweka shinikizo katika mwelekeo huu,” ameongeza Bw. Conille. Waziri Mkuu huyo wa muda alizuru Kenya wiki moja baada ya shambulizi kali la genge lililoua watu 109 na kuwajeruhi zaidi ya arobaini.
Wanachama wa genge lililojihami kwa silaha waliwafyatulia risasi wakaazi katika mji wa Pont-Sondé, ulioko takriban kilomita 100 kaskazini-magharibi mwa mji mkuu Port-au-Prince, wakiteketeza makumi ya nyumba na magari. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongeza muda wa ujumbe wa polisi wa kimataifa kwa mwaka mwingine mwezi uliopita, bila kutaja uwezekano wa kubadilishwa kwake kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa kama ilivyoombwa na mamlaka mpya ya nchi hiyo.
Haiti imeteseka kwa muda mrefu kutokana na ghasia za makundi hayo yenye silaha, ambayo yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu wa Port-au-Prince na barabara kuu za nchi hiyo. Takriban watu 3,661 wameuawa tangu mwezi wa Januari nchini Haiti, iliyoathiriwa na ghasia, kulingana na takwimu iliyotajwa mwishoni mwa mwezi wa Septemba na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu.
Wimbi la ghasia na hali mbaya ya kibinadamu imewalazimu zaidi ya watu 700,000, nusu yao wakiwa watoto, kukimbia makazi yao na kutafuta hifadhi kwingineko nchini humo, kwa mujibu wa takwimu za hivi punde za Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
UN: Zaidi ya watu nusu milioni wasio na uraia wamepata uraia ndani ya miaka kumi
Katika ripoti iliyotolewa mjini Geneva, UNHCR imeeleza maendeleo yaliyopatikana tangu kuzinduliwa mwaka 2014 kwa kampeni ya #IExist, ambayo inalenga kuhamasisha hatua za kimataifa kutatua tatizo la watu wasio na uraia.
Imechapishwa: 11/10/2024 – 16:25
Dakika 2

UNHCR inaelezea kutokuwa na uraia kama “ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu”.
Hali hiyo inaweka watu pembeni kisiasa na kiuchumi, inawafanya wawe katika hatari ya kunyanyaswa na kutumiwa, na inawanyima kupata huduma muhimu.
Mnamo mwaka wa 2023, UNHCR iliripoti watu milioni 4.4 wasio na uraia, huku ikisisitiza kuwa mamilioni ya watu wengine waliathiriwa kwa sababu data zilizopo zilifikia nusu ya nchi ulimwenguni.
Kampeni hiyo, ambayo itakamilika mwaka huu, inalenga kudhibiti “mgogoro usioonekana kwa kiasi kikubwa, wa mamilioni ya watu duniani kote wanaoishi katika vivuli, bila uraia, ambao hawawezi kudai haki zao za kimsingi za kibinadamu “, amesisitiza Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi Filippo Grandi.
Ingawa “maendeleo makubwa” yamefanywa kumaliza hali hii, “kazi yetu bado haijakamilika,” amesema.
Kulingana na ripoti hiyo, “zaidi ya watu 565,900 wasio na uraia na watu wasio na utaifa maalum wamepata uraia” katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
‘maendeleo ya ajabu’
Mwigizaji wa Australia Cate Blanchett, balozi wa nia njema wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Wakimbizi, amesema maendeleo yalikuwa “ya kushangaza”.
“Nchi 20 zimeboresha haki za watu wasio na uraia, nchi kumi na tatu zimetunga sheria kuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayezaliwa bila uraia,” ameongeza.
“Lazima tuhakikishe kuwa kila mtu ambaye bado anaishi bila uraia au utaifa anapewa haki ya kutambuliwa na sio kutengwa,” amesisitiza.
UNHCR imebainisha juhudi katika nchi zikiwemo Turkmenistan, Ureno, Macedonia Kaskazini, Rwanda, Brazil na Thailand.
Kyrgyzstan imesuluhisha kesi zote zinazojulikana za watu wasio na uraia katika eneo lake, UNHCR inasisitiza.
Aidha, nchi 77 zimejiunga na mikataba ya Umoja wa Mataifa kuhusu kutokuwa na uraia, na angalau nchi 22 zimepitisha mipango ya kumaliza tatizo la ukosefu wa uraia.
“Mafanikio makubwa yamepatikana ili kukabiliana na janga hili baya, lakini hitaji la kuendelea kuchukua hatua bado ni muhimu,” amesema Ruven Menikdiwela, Naibu Kamishna Mkuu anayehusika na masuala ya ulinzi.
“Bado kuna idadi kubwa ya watu ambao hawapo kwenye karatasi, na wanasukumwa pembezoni mwa jamii, kwa sababu tu ya ubaguzi wa kikabila, kidini au kijinsia, au kwa sababu ya mapungufu katika sheria na kanuni kuhusu sera za uraia,” almesema. .
UNHCR imesema itafanya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu tatizo la watu wasio na uraia mjini Geneva siku ya Jumatatu.
Pia imetangaza kuzinduliwa kwa “Muungano wa Kimataifa wa Kukomesha Ukosefu wa Uraia.”
Israeli yashambulia kikosi cha UNIFIL kusini mwa Lebanon, walinda amani kadhaa wajeruhiwa
Umoja wa Mataifa umeripoti kwamba Israel imeshambulia tena makao makuu ya kikosi cha umoja wa Mataifa nchini Lebanoni UNIFIL kusini mwa Lebanon.

Vikosi vya Israel vimeshambulia kituo cha uchunguzi cha kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (UNIFIL) kwenye makao yake makuu katika mji wa Naqoura kusini mwa Lebanoni siku ya Ijumaa, na kujeruhi watu wawili, chanzo cha Umoja wa Mataifa kimesema. Vikosi vya Israel pia vimeingia katika eneo lingine linalokaliwa na UNIFIL ambalo lilishambuliwa siku ya Alhamisi, chanzo hicho kimeongeza. Walinda amani wapatao 10,000 wametumwa kusini mwa Lebanoni.
Shambulio jipya la Israel limelenga makao makuu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (UNIFIL) kilochutumwa kati ya kusini mwa Lebanoni na mpaka wa Israel. Tukio hilo limetokea siku ya Ijumaa, shambulio ambalo limewajeruhi walinda amani wawili. Siku ya Alhamisi, walinda amani wa Indonesia walijeruhiwa baada ya kurushiwa risasi na wanajeshi wa Israel.
China ‘inalaani vikali’ shambulio la Israel dhidi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanoni
China “imeshutumu vikali” siku ya Ijumaa ufyatuaji risasi wa Israel ambao, kulingana na Umoja wa Mataifa, umelenga makao makuu ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanoni, wakitaka uchunguzi ufanyike na kutaka “kupungua” kwa uhasama. “China inaelezea wasiwasi wake mkubwa na inalaani vikali shambulio la jeshi la Israeli kwenye nafasi na vituo vya uchunguzi vya UNIFIL”, Jeshi la Muda la Umoja wa Mataifa nchini Lebanoni ametangaza msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mao Ning.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.