Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kitatoa tahadhari kwa raia wa Marekani kusafirinchini Rwanda, na kupendekeza raia kuepuka safari zisizo za lazima kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg katika nchi hiyo ya Afrika mashariki, serikali ya Marekani imesema.
CDC itaanza kuwachunguza wasafiri wanaoingia Marekani ambao wamekuwa Rwanda katika siku 21 zilizopita, Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani imesema.
Wiki iliyopita, kituo hiki kilitoa tahadhari yake ya kwanza kwa raia wa Marekani kusafiri nchini Rwanda, ikitaka tahadhari kuimarishwa kwa wale wanaosafiri kwenda nchini humo.
Mlipuko wa kwanza wa ugonjwa kama Ebola nchini Rwanda uligunduliwa mwishoni mwa mwezi wa Septemba mwaka huu baada ya kuripotiwa wagonjwa 46 na vifo 12 tangu wakati huo. Marburg inaua kwa 88%.
Huambukizwa kwa binadamu na popo wa matunda na kisha huenea kwa kugusana na umajimaji wa mwili wa watu walioambukizwa.
Rwanda imeanza kutoa dozi za chanjo dhidi ya virusi hivyo, ikiweka kipaumbele katika hatari zaidi, wafanyakazi wengi wa afya walio katika hatari ya kuambukizwa, na wale wanaokaribiana na wagonjwa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.