Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja
Muhtasari
- Raia wa Afghanistan akamatwa kwa madai ya njama ya shambulizi siku ya uchaguzi wa Marekani
- Urusi inadhamiria kusababisha ghasia katika maeneo ya Uingereza, inaonya MI5
- Jimbo la Florida Marekani lajitayarisha kukabiliana na kimbunga Milton
Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Asubui ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 09/10/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.
Raia wa Afghanistan akamatwa kwa madai ya njama ya shambulizi siku ya uchaguzi wa Marekani

Wizara ya Sheria ya Marekani imemkamata mtu anayedaiwa kupanga shambulizi siku ya Uchaguzi na anahusishwa na kundi la Islamic State.
Mshukiwa, Nasir Ahmad Tawhedi, 27, ni raia wa Afghanistan anayeishi katika mji wa Oklahoma, kulingana na waendesha mashtaka.
Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray alisema katika taarifa ya Jumanne kwamba: “Mshtakiwa huyu, akichochewa na ISIS, alikula njama ya kufanya shambulio la kikatili, Siku ya Uchaguzi, hapa nchini kwetu.”
FBI ilisema alikuwa akijaribu kuhifadhi silaha, na alikuwa amechukua hatua kuuza mali za familia yake na kuwahamisha wanafamilia wake nje ya nchi.
Bw Tawhedi anashtakiwa kwa kutoa, kujaribu kutoa, na kula njama ya kusaidia au kutoa rasilimali kwa shirika la kigeni la kigaidi; na kwa kujaribu kununua bunduki na risasi za kutumia kufanya uhalifu au kitendo cha kigaidi.
FBI ilisema Bw Tawhedi alifanya kazi na mwenzake ambaye jina lake halikutajwa, jamaa wake mwenye umri mdogo na pia ni raia wa Afghanistan.
Inamtuhumu kwa kutumia propaganda za Islamic State kupitia mtandao, kulingana na rekodi za Google zilizopatikana na vyombo vya sheria, na kutoa michango kwa shirika la kutoa msaada linalotumika na IS.
“Tutaendelea kupambana na tishio linaloendelea ambalo ISIS na wafuasi wake wanaleta kwa usalama wa taifa wa Marekani, na tutawatambua, kuwachunguza na kuwafungulia mashtaka watu wanaotaka kuwatisha watu wa Marekani,” alisema Mwanasheria Mkuu Merrick Garland.
Bw Tawhedi alitafuta bunduki aina ya AK-47 ili kutumia katika shambulio hilo, mamlaka zinadai.
Mnamo tarehe 7 Oktoba, yeye na mwanzilishi mwenza walikutana na watu ambao kwa kweli walifanya kazi kwa siri kwa FBI kununua silaha na risasi.
Baada ya ununuzi huo, Bw Tawhedi na mshiriki mwenzake walikamatwa.
Bw Tawhedi aliwasili Marekani mnamo Septemba 2021 kwa visa maalum ya wahamiaji pamoja na mkewe na mtoto wake mdogo.
Alikuwa anaishi katika mji wa Oklahoma wakati wa kukamatwa kwake.
Haijabainika mara moja ikiwa ana uwakilishi wa kisheria.
Urusi inadhamiria kusababisha ghasia katika mitaa ya Uingereza, inaonya MI5

Shirika la kijasusi la Urusi limekuwa likifanyia kazi suala la kuhakikisha kuna “ghasia endelevu katika mitaa ya Uingereza na Ulaya”, mkuu wa MI5 amesema.
Akitoa taarifa yake ya kila mwaka kuhusu vitisho vya usalama vinavyoikabili Uingereza, Ken McCallum alisema maafisa wa ujasusi wa GRU waliendeleza vitendo vya “uchomaji moto, hujuma na vingine vya hatari zaidi pamoja na kuongezeka kwa uzembe” nchini Uingereza baada ya nchi hiyo kuunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi.
MI5 pia imejibu njama 20 zilizoungwa mkono na Iran tangu 2022, alisema, ingawa aliongeza kuwa kazi zake nyingi bado zinahusisha itikadi kali za Kiislamu na kufuatiwa na ugaidi uliokithiri wa mrengo wa kulia.
Mchanganyiko wa vitisho vinavyohusiana na ugaidi kutoka kwa mataifa ulimaanisha MI5 ilikuwa na “kazi moja walioyoipa kipaumbele”, alionya.
Katika hotuba yake ya wigo mpana, alisema:
- Vijana walikuwa wakivutiwa zaidi na itikadi kali mtandaoni, huku 13% ya wale waliochunguzwa kwa kuhusika na ugaidi walikuwa na umri wa chini ya miaka 18.
- Jumla ya njama 43 zilizofanywa dakika za mwisho zilihusisha bunduki na vilipuzi kwa nia ya kutekeleza “mauaji ya watu wengi” nchini Uingereza zilizuiliwa tangu 2017
- Uchunguzi wa vitisho dhidi ya serikali uliofanywa na MI5 uliongezeka kwa 48%
- Kazi ya kukabiliana na ugaidi imesalia katika pande mbili kati ya “asilimia 75 ya Waislamu wenye msimamo mkali, na 25% ni ugaidi uliokithiri wa mrengo wa kulia”
Pia kulikuwa na “imani na itikadi mchanganyiko” na ilibidi MI5 kukabiliana nazo, aliambia mkutano huo katika kituo cha oparesheni za kukabiliana na ugaidi cha MI5 huko London.
Jimbo la Florida Marekani lajitayarisha kukabiliana na kimbunga Milton

Wakazi wa eneo la Florida wanaharakisha kumaliza maandalizi ya dharura – au waondoke tu – huku Kimbunga Milton kikielekea kwa haraka kwenye Ghuba ya Tampa iliyo na watu wengi.
Milton kwa sasa ni dhoruba ya aina ya tano, yenye upepo mkali wa hadi 165mph (270km/h).
Kinatarajiwa kupiga kwa nguvu zote Jumatano usiku, chini ya wiki mbili baada ya jimbo hilo kukumbwa na kimbunga cha Helene.
Rais Joe Biden alionya watu huko Florida Jumanne kuondoka makwao na kulichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa kama lenye kuhusisha “maisha au kifo” wakati jimbo hilo likijitahidi zaidi kwenye uhamishaji.
Kimbunga hicho kikiwa kimewekwa “kitengo cha tano, ni kama kimbunga kikubwa,” mkazi mmoja wa jiji la Ghuba la Bradenton aliambia BBC kutoka hoteli ambayo amehamia Kissimmee.
“Nisingependa kuwa huko,” alisema Gerald Lemus. “Hii itakuwa dhoruba isiyokifani haijalishi itakumba wapi.”
Bw Lemus, ambaye ameishi Bradenton maisha yake yote, alisema hajawahi kuhama kutokana na dhoruba zilizotangulia. Lakini aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wa binti yake wa miaka minane.
“Nilimtazama tu na sikuweza kumtia mashaka kwa kitu kama hiki,” alisema Jumanne usiku.
“Ni hatua ya hatari ambayo hatukutaka kuichukua.”
ML Ferguson amekuwa akihangaika kujenga upya nyumba yake huko Anna Maria, Florida, baada ya kuharibiwa vibaya mwezi uliopita na kimbunga Helene, ambacho kilikuwa kikali kilichowekwa kwenye kitengo cha nne.
“Hiki kitakuwa kibaya zaidi kuliko Helene,” alisema kwenye simu akiwa katika barabara kuu nje ya jiji.
“Gari langu limeharibika kiasi cha kutoweza kutengenezeka tena, sote tulifutwa kazi, na mali [zangu] ziliharibiwa. Baada ya dhoruba hii kupiga, itakuwa rasmi sasa sina makazi.”
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024r
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.