Mkuu wa diplomasia ya Rwanda aishutumu DRC kwa kuvuruga mazungumzo ya Luanda

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa DRC Félix Tshisekedi wa Kongo na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikaribiana kwa mita chache kwenye picha ya familia iliyofungua mkutano wa kilele wa Francophonie, siku ya Ijumaa huko Villers-Cotterêts, kaskazini mwa Paris, lakini viongozi hao wawili hawakuzungumza. Kinshasa inaishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23. 

Picha ya wakuu wa nchi walioshiriki katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Francophonie, huko Château de Villers-Cotterets, kaskazini-mashariki mwa Ufaransa, Oktoba 4, 2024. Rais wa DRC Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikaribiana mita chache, lakini hawakuzungumza.
Picha ya wakuu wa nchi walioshiriki katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Francophonie, huko Château de Villers-Cotterets, kaskazini-mashariki mwa Ufaransa, Oktoba 4, 2024. Rais wa DRC Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikaribiana mita chache, lakini hawakuzungumza. AFP – LUDOVIC MARIN

Wakati wa mkutano wa kilele wa OIF, Rais Tshisekedi hakufurahia jinsi rais wa Ufaransa hakuzungumzia mzozo wa mashariki mwa DRC katika hotuba yake ya ufunguzi. Ni katika hali hiyo ambapo, Jumamosi Oktoba 5, mkuu wa diplomasia ya Rwanda, Olivier Nduhungirehe, aliishutumu DRC kwa kuvuruga mazungumzo ya amani ya Luanda.

Mzozo mkubwa wa kidiplomasia na kijeshi kati ya nchi zao mbili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), eneo linalokumbwa na miongo kadhaa ya ghasia, bado unaendelea, licha ya matumaini ya Paris kuona viogozi hao wakisogeleana wakati wa picha ya pamoja ya viongozi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa OIF.

Mara baada ya wazo la mkutano kati ya Paul Kagame na Félix Tshisekedi halikuweza kutekelezwa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, mwenyeji wa mkutano huo, hatimaye alizungumza na kila mmoja kati ya viongozi wenzake wawili kwa wakati tofauti “kuwahimiza” kuhitimisha makubaliano ya amani “haraka iwezekanavyo”, wakati Angola, mpatanishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika, imekuwa akijaribu kwa miezi kadhaa kupata maendeleo katika suala hili nyeti.

DRC, pamoja na kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa, wanaishutumu Rwanda kwa kupeleka wanajeshi kuunga mkono M23 (March 23 Movement), ambayo imeteka maeneo makubwa ya eneo katika eneo hili tajiri kwa madini tangu mwaka 2021.

Mgogoro wa mashariki mwa DRC umefichua mvutano mkubwa wa ndani. Rais wa Kongo Félix Tshisekedi alisusia kikao cha faragha cha wakuu wa nchi Jumamosi alasiri, Oktoba 5, na pia hakushiriki chakula cha mchana kilichotolewa adhuhuri na Louise Mushikiwabo, katibu mkuu wa OIF. Katika suala hili: hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Emmanuel Macron. Alipozungumzia migogoro duniani kote, rais wa Ufaransa hakutaja mzozo wa mashariki mwa DRC.

Siku ya Jumamosi jioni, Emmanuel Macron alitoa wito kwa “waasi wa M23 na wanajeshi wa Rwanda kuondoka” katika ardhi ya Kongo, kama ilivyotakiwa na Kinshasa: “Tunatoa wito kwa waasi wa M23 na wanajeshi wa Rwanda kuondoka haraka mashariki mwa DRC. Pia tunatoa wito wa kuvunjwa kwa FDLR na makundi yote yenye silaha nchini DRC, na kukomeshwa kwa matamshi ya chuki. “

Ni katika muktadha huu ambapo mkuu wa diplomasia ya Rwanda, Olivier Nduhungirehe, aliishutumu DRC kwa kuvuruga mijadala ya Luanda.

Mkutano wa mwisho wa mawaziri mnamo Septemba 14 ulikuwa wa kuahidi, ningesema, kwa kuwa kulikuwa na mpango uliooanishwa wa kuwatenganisha FDLR na kuondoa hatua zetu za ulinzi wa Rwanda. Mpango huu ulikuwa umepatanishwa na wataalamu kutoka nchi hizo tatu, akiwemo mtaalamu kutoka DRC. Katika mkutano wa Septemba 14, wataalamu hao watatu, akiwemo mkuu wa ujasusi wa kijeshi wa DRC, waliunga mkono mpango huu na kumtaka Waziri Mkuu kuupitisha. Kwa hivyo, Rwanda ilikubali na waziri wa DRC alipinga, kwani baadaye pia alipinga mazungumzo yoyote ya kisiasa na M23 ili kusuluhisha swali hilo kwa uhakika, wakati Rwanda ilitaka kuwe na mazungumzo ya kushughulikia sababu za mgogoro huo. Kwa hiyo, ni DRC iliyozuia mchakato huu. Sasa Angola imetualika kwa mkutano wa 5 wa mawaziri mnamo Oktoba 12. Tunasubiri kuona ajenda haswa, lakini tunaamini kwamba ni juu ya DRC, sasa, kuunga mkono kikamilifu mchakato huu wa Luanda.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment