Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa
Raia nchini Kenya na hasa wale wa kawaida wanaotegemea kupata matibabu katika hospitali za uma na zile za binafsi, wako katika sintofahamu, baadhi wakishindwa kuhudumiwa chini ya mfumo mpya wa bima ya afya kwa wote, SHIF.

Mfumo huu mpya ambao ulianza kutumiwa rasmi Octoba mosi, unachukua nafasi ya ule wa zamani uliokuwa unafahamika kama NHIF.
Hata hivyo, jana kwa siku ya pili mfululizo mtandao wa mfumo huo hasa wa kuhuisha takwimu za watumiaji, ulikuwa haufanyi kazi hali iliyowalazimu baadhi ya raia kutumia fedha zao binafsi kupata matibabu.
Ripoti zinaonesha kuwa baadhi ya hospitali binafsi zilikataa kuwahudumia raia waliojisajili chini ya mfumo mpya, kwa kile viongozi wao wanasema wana wasiwasi kuwa huenda madeni yao yaliokuwa chini ya NHIF yasilipwe kupitia mfumo mpya wa SHIF.
Ili kuonyesha maudhui haya X (Twitter) maudhui, unahitaji kuidhinisha kipimo cha hadhira na vidakuzi vya matangazo.KubaliDhibiti chaguo langu
Hata hivyo licha ya changamoto zinazoendelea kujitokeza ikiwemo raia kushindwa kutumia huduma ya ujumbe mfupi kuangalia ikiwa taarifa zao zimehuishwa katika mfumo wa sasa, Serikali imewatoa hofu ikisisitiza kuendelea na zoezi la usajili huku changamoto zilizojitokeza zikiendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Hapo jana kupitia mitandao ya kijamii raia wengi walilalamika kuhusu kushindwa kupata huduma chini ya mfumo huu ambao umeibua maswali kuhusu ufanisi wake hasa kutokana na shida zilizoshuhudiwa chini ya mfumo wa NHIF.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.