Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mkuu wa mpya wa muungano wa NATO, Mark Rutte amezuru nchi ya Ukraine, ziara inayotajwa kuwa ishara ya mshikamano na Kyiv wakati huu ikiendelea na mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Kyiv inategemea msaada wa mabilioni ya Dolla kutoka kwa washirika wake mataifa ya Magharibi katika vita vyake dhidi ya uvamizi wa Moscow.
Mark Rutte, Waziri Mkuu wa zamani wa Uholanzi anachukua wadhifa wa katibu Mkuu wa NATO wakati huu ambapo Urusi inaripotiwa kuendelea kupiga hatua katika uwanja wa mapambano, uchaguzi wa Marekani ukiwa unakaribia katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Katibu huyo Mkuu mpya wa NATO ameahidi kwamba muungano wa NATO utaendelea kusimama na nchi yake Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi chini ya uongozi wake.
“Putin anastahili kufahamu kwamba hatutachoka na kwamba Ukraine mwishowe itashinda,”alisema baada ya kuchukua wadhifa wa kioongoza NATO.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa upande wake ameeleza kuridhishwa na uteuzi wa Mark Rutte kuwa katibu Mkuu wa NATO.
Aidha Rutte amesisitiza kwamba mpango wa Ukraine kupata uanachama wa NATO na suala ambalo haliwezi kusahaulika na kwamba ni lazima litimie.
Wakati akiwa Waziri Mkuu wa Uholanzi, serikali yake ilionekana kuwa mojawapo ya mataifa yenye mchango mkubwa kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi, akishinikiza Kyiv kupewa ndege za kivita aina na F-16.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.