Watu 45 wamefariki baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuzama pwani ya Djibouti

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji, IOM, limesema watu 45 wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya bahari ya Djibouti.

Mamia ya raia wa Afrika hutumia njia hatari kusafiri kwenda Ulaya kwa ajili ya kutafuta maisha bora.
Mamia ya raia wa Afrika hutumia njia hatari kusafiri kwenda Ulaya kwa ajili ya kutafuta maisha bora. © AFP

Kwa mujibu wa shirika hilo, boti hiyo iliyotokea Yemen ilikuwa na wahamiaji zaidi ya 300, ambapo mpaka sasa watu 32 pekee ndio wamefanikiwa kuokolewa wakati huu pia operesheni ya uokoaji ikiendelea.

Tukio hili kwenye pwani ya Djibouti, linajiri siku chache kupita tangu wahamiaji 12 wapoteze maisha katika pwani ya nchi ya Tunisia, baada ya boti kuzama wakijaribu kuelekea Ulaya kupitia bahari ya Mediterania.

Soma piaWahamiaji haramu tisa wafariki baada ya boti lao kuzama katika Visiwa vya #canary

Katika hatua nyingine, tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, imesema nchi ya Tunisia imerudi nyuma katika ulinzi wa haki za wahamiaji, wakati huu dazeni ya wanaharakati wa haki za binadamu wakikamatwa.

Nchi ya Tunisia na jirani yake Libya, zimekuwa njia kuu za wahamiaji wanaojaribu kuelekea barani Ulaya.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment