Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa
Watu zaidi ya 700,000 wamekimbia makaazi yao nchini Haiti, nusu wakiwa ni watoto, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa siku ya Jumatano na Umoja wa Mataifa.

Sababu kubwa inayosababisha watu nchini Haiti hasa katika jiji kuu Port-au-Prince, kukimbia makaazi yao ni kwa sababu za kiusalama kutokana na uwepo wa magenge yaliyojihami kwa silaha, yanayoendelea kuwahangaisha wakaazi.
Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wahamiaji IOM imesema kufikia mwisho wa mwezi wa Septemba watu 702,973 walikuwa wamekimbia makaazi yao.
Hili ni ongezeko la asilimia 22 la watu waliokimbia, tangu mwezi Juni, wakati huu pia hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbaya kwa sababu ya ukosefu wa chakula.

Aidha, imebainika kuwa asilimia 83 ya wakimbizi hao wamepewa hifadhi na ndugu zao, na mbali na ukosefu wa chakula, wakimbizi hao wanakabiliwa na ukosefu wa huduma za afya.
Ijumaa iliyopita, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, iliripotiwa kuwa watu 3,600 wameuawa mwaka huu nchini Haiti baada ya kushambuliwa na magenge yenye silaha, wakati huu kikosi cha polisi wa Kimataifa kikiongozwa na Kenya, kikijaribu kupambana na magenge hayo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.