DRC: Kampeni ya utoaji wa chanjo ya Mpox yahairishwa kwa mara nyengine

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Mamlaka nchini DRC kwa mara nyingine zimeahirisha kuanza kampeni ya utoaji chanjo dhidi ya virusi vya Mpox, ambavyo vimesababisha vifo vya mamia ya raia wa nchi hiyo wakati huu maambukizo zaidi yakiripotiwa.

DRC ilikuwa imepanga kuanzisha zoezi la uchomaji wa chanjo hiyo tarehe mbili ya mwezi huu.
DRC ilikuwa imepanga kuanzisha zoezi la uchomaji wa chanjo hiyo tarehe mbili ya mwezi huu. © AFP

Akinukuliwa na shirika la habari la AFP, afisa wa juu kwenye wizara ya afya nchini DRC, Nanou Yanga, amesema hawatarajii kuanza kampeni hiyo hivi leo kama ilivyokuwa imetangazwa awali kwa kile amesema kuna haja ya mafunzo na elimu zaidi kutolewa kwa wahudumu wa afya na raia.

Kwa mujibu wa Dr Yanga, kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo itaanzia mashariki mwa nchi hiyo ambako kumeripotiwa idadi kubwa ya maambukizo, bila hata hivyo kutaja tarehe nyingine.

Chanjo ya mpox ikiwasili jijini Kinshasa kutoka kwa Umoja wa Ulaya  Tarehe 5 ya mwezi  Septemba 2024.
Chanjo ya mpox ikiwasili jijini Kinshasa kutoka kwa Umoja wa Ulaya Tarehe 5 ya mwezi Septemba 2024. © EUROPEAN UNION / AFP

Aidha Dr Yanga methibitisha chanjo kuwasili Jumatatu ya wiki hii kwenye mji wa Bukavu jimboni Kivu Kusini na kuongeza kuwa kampeni ya chanjo itaanza ndani ya wiki moja ijayo.

Agosti 14 mwaka huu shirika la afya duniani liliutangaza ugonjwa wa Mpox kama janga la dharura la kiafya duniani, huku nchi ya DRC likiwa taifa lenye idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa Mpox barani Afrika.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment