DRC: Augustin Kabuya wa chama cha rais, UDPS, aomba marekebisho ya Katiba

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Mjadala kuhusu Katiba unaibuka tena nchini DRC. Augustin Kabuya, Katibu Mkuu wa UDPS, alitoa matamshi hayo wakati wa mkutano maarufu mwishoni mwa juma lililopita ambao ulizua mzozo mkali ndani ya makundi ya wanasiasa na mashirika ya kiraia, kwa kuibua hoja ya marekebisho ya Katiba.

Augustin Kabuya, mkuu wa chama cha rais na mtoa habari katika Bunge la taifa la DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Februari 15, 2024.
Augustin Kabuya, mkuu wa chama cha rais na mtoa habari katika Bunge la taifa la DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Februari 15, 2024. © Pascal Mulegwa/RFI

Katika hotuba yake, Augustin Kabuya aliomba marekebisho ya Katiba, akibaini kwama ina mapungufu kadhaa. Kulingana na Bw. Kabuya, miaka mitano ya muhula wa rais haifai. Sehemu ya kipindi hiki ilitolewa, alisema, kwa mazungumzo ya kuunda serikali. Hii inapunguza muda halisi wa muhula wa rais hadi karibu miaka mitatu.

Augustin Kabuya pia alikosoa chimbuko la Katiba, akisema kwamba “ilitengenezwa na wageni”, hoja anayotumia kuhalalisha mwito wake wa marekebisho.

Kauli hizi zimeshutumiwa haraka na mashirika kadhaa ya kiraia na wapinzani. Kwa mfano, shirika lisilo la kiserikali la Justicia ASBL limejibu kwa kumshutumu Augustin Kabuya kwa kuleta mkanganyiko kimakusudi kati ya marekebisho na mabadiliko ya Katiba. Hali ambayo, kulingana na shirika hilo, ni ukiukaji wa Ibara ya 220, ambayo inalinda vipengele muhimu, kama vile ukomo wa mihula ya rais.

Kwa upande wake, Rais Tshisekedi, Agosti mwaka jana, alikanusha nia yoyote ya kurekebisha Katiba ili kuongeza muhula wake, akibainisha: “Sijawahi kusema kwamba nitabadilisha Katiba ili kuongeza muda wa muhula wangu. Haya ni masharti yasiyobadilika, na watu lazima washauriwe kabla ya kufanya marekebisho yoyote. “

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment