Boti za doria pamoja na helkopta zimeendelea na zoezi la kuwatafuta wakimbizi na wahamiaji 48 ambao hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya kisiwa cha El Hierro nchini Hispania.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa
Hata hivyo kwa mujibu wa mamlaka kwenye kisiwa hicho, matumaini ya kuwapata watu hao wakiwa hai hayapo wakati huu wakifanikiwa kupata miili 9 ikiwemo ya mtoto mmoja.
Katika operesheni hiyo iliyoanza majira ya asubuhi ya Jumamosi iliyopita, ilifanikisha kuwaokoa watu 27 kati ya 84 waliokuwa wakijaribu kufika kwenye kisiwa cha El Hierro magharibi mwa Visiwa vya Canary.
Viongozi kwenye kisiwa maarufu cha Canary, ambacho ni kituo kikuu cha wahamiaji, wamesema boti hiyo ilikuwa imebeba raia kutoka Mali, Mauritania na Senegal wakati ikizama.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.