Iran inasema haitowatuma wanajeshi wake kupigana nchini Lebanon na Gaza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Iran kupitia Wizara yake ya mambo ya kigeni inasema haitawatuma wanajeshi wake nchini Lebanon au katika Ukanda wa Gaza kupigana dhidi ya wanajeshi wa Israeli.

Rais wa Iran  Masoud Pezeshkian.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian. AP – Pamela Smith

Taarifa ya Iran inakuja wakati huu Israeli ikiripotiwa kuendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya ngome za washirika wa Tehran mashariki ya kati.

Israel katika siku za hivi karibuni imekuwa ikitekeleza mashambulio mazito ya angani nchini Lebanon kuwakabili wapiganaji wenye silaha inayosema wanaungwa mkono na Iran katika eneo la mashariki ya kati ikiwemo SyriaYemen na Iraq.

Tangazo hili linakuja baada ya shambulio la Israeli la Ijumaa ya wiki iliopita kumuua kiongozi wa wapiganaji Hezbollah Hassan Nasrallah.

Soma piaLebanon: Kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah ameuuawa na Israeli

Kundi hilo lenye silaha kwa muda mrefu limekuwa likiuungwa mkono na serikali ya Iran.

Katika hatua nyengine, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ametembelea ofisi ya Hezbollah mjini Tehran kutoa heshima zake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa kundi hilo Hassan Nasrallah kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa serikali ya Iran.

Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye yupo na usemi mkubwa katika maamuzi ya serikali amesema maujai ya Nasrallah yatajibiwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment