Afrika: Raia katika nchi 21 hawana imani na zoezi la uchaguzi kwenye mataifa yao

Nchi 21 barani Afrika zilishuhudia kushuka, kwa kiwango kikubwa, uaminifu wa uchaguzi kati ya mwaka 2020 na 2024, kulingana na ripoti ya Hali ya Demokrasia Duniani ya mwaka 2024 iliyoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://liveonlineradio.net/radio-fortune-africa

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, migogoro barani imechangia kushuka kwa imani ya umma katika michakato ya kisiasa
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, migogoro barani imechangia kushuka kwa imani ya umma katika michakato ya kisiasa REUTERS/Edward Echwalu

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mpiga kura mmoja kati ya watatu barani atapiga kura mwaka huu katika taifa ambalo ubora wa zoezi la Uchaguzi ni mbaya sana kuliko miaka mitano iliyopita.

Kati ya mwaka wa 2020 na katikati ya mwaka huu, uchaguzi mmoja kati ya tano ulipingwa mahakamani, huku zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vikiibuka kama vipengele vinavyolalamikiwa zaidi.

Katika kipindi hicho, uchaguzi mmoja kati ya tano ulishuhudia mgombea wa Urais aliyeshindwa au chama kilichopoteza katika chaguzi za ubunge kikikataa hadharani matokeo ya uchaguzi huo, na vyama vya upinzani vikisusia uchaguzi mmoja katika chaguzi 10.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, migogoro barani imechangia kushuka kwa imani ya umma katika michakato ya kisiasa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment