Mshindi wa Dhahabu ya Olimpiki, Joshua Cheptegei kushiriki Mbio za Vedanta Delhi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore

Cheptegei atanatazamiwa kuweka rekodi katika mbio hizo, baada kushinda dhahabu katika riadha mbio za mita 10,000 katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.Peres Jepchirchir ni bingwa mara tatu wa dunia wa nusu marathon. Hivi majuzi alishinda mbio za London Marathon 2024, na kuvunja rekodi pekee ya ulimwengu ya marathon kwa wanawake.

Joshua Cheptegei célèbre sa victoire sur le 10 000 mètres, le 2 août 2024.
Joshua Cheptegei célèbre sa victoire sur le 10 000 mètres, le 2 août 2024. AFP – JEWEL SAMAD

Mshindi wa medali ya dhahabu katika olimpiki ya paris mwaka huu raia wa Uganda, Joshua Cheptegei ni baadhi ya wanariadha wanaotazamiwa kuongoza wanariadha wengine katika mbio za Vedanta Delhi nusu Marathon zinazopangwa kufanyika Oktoba 20.

Mwanariadha wa Kenya Joshua Cheptegei baada ya kushinda dhahabu ya mita 10,000
Mwanariadha wa Kenya Joshua Cheptegei baada ya kushinda dhahabu ya mita 10,000 © Word Athletics

Cheptegei atanatazamiwa kuweka rekodi katika mbio hizo, baada kushinda dhahabu katika riadha mbio za mita 10,000 katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Ili kuonyesha maudhui haya X (Twitter) maudhui, unahitaji kuidhinisha kipimo cha hadhira na vidakuzi vya matangazo.KubaliDhibiti chaguo langu

Raia huyo wa Uganda, pia anashikilia rekodi za dunia za mbio za mita 5,000 na 10,000 na ana historia ya ajabu ya mafanikio ya kimataifa, akishinda medali kadhaa za dhahabu katika mashindano ya Jumuiya ya Madola.

Rekodi ya kupendeza ni kuwa, Cheptegei alikimbia mbio zake za kwanza kimataifa nchini India katika TCS World 10K Bengaluru 2014, na kumaliza wa pili. Kurudi kwake kunaahidi kuwa ni kivutio cha mbio za mwaka huu.

Mkenya Peres Jepchirchir, atajiunga na Cheptegei katika mbio hizo akishiriki kwa upande wa kinadada.

Peres Jepchirchir of Kenya crosses the finish line to win the women-only half marathon in a new record time
Peres Jepchirchir of Kenya crosses the finish line to win the women-only half marathon in a new record time AFP

Peres Jepchirchir ni bingwa mara tatu wa dunia wa nusu marathon. Hivi majuzi alishinda mbio za London Marathon 2024, na kuvunja rekodi pekee ya ulimwengu ya marathon kwa wanawake.

Ili kuonyesha maudhui haya X (Twitter) maudhui, unahitaji kuidhinisha kipimo cha hadhira na vidakuzi vya matangazo.KubaliDhibiti chaguo langu

Mbio hizo za Vedanta Delhi nusu Marathon zitatoa jumla ya dola ya marekani 260,000 pesa za zawadi. Pia zinatarajiwa kuwa kivutio cha kalenda ya mbio za India mwaka huu.

Vedanta Delhi Half Marathon, ni sehemu ya mashindano ya dunia ya riadha za barabara yenye dhamani ya dhahabu, zitapeperushwa kutoka Uwanja wa Jawaharlal Nehru Jumapili, Oktoba 20.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment