Afrika Leo Jioni.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore

Muhtasari

  • Putin achora mstari mwekundu wa nyuklia kwa nchi za Magharibi
  • Shambulizi la Israel lawauwa wanajeshi 5 katika mpaka wa Syria na Lebanon
  • Ukraine yasema ndege zisizo na rubani 24 za Urusi zimedunguliwa huku moja ikiingia Romania
  • IDF yadai kuwaua viongozi wengine wakuu zaidi wa Hezbollah katika shambulizi lililopita
  • Shambulizi laua wanafamilia tisa nchini Lebanon – ripoti
  • Mamlaka ya Lebanon yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja
  • Mazungumzo ya kusitisha mapigano yataendelea hata kama mapigano yanaendelea – Netanyahu
  • Alabama yatekeleza hukumu ya kifo ya pili ya gesi ya nitrojeni
  • Trump na Zelensky kukutana huku wanachama wa Republican wakiwa na hasira
  • Naomi Campbell apigwa marufuku kuwa mdhamini wa shirika la kutoa misaada
  • Israel yaishambulia Hezbollah kwa ‘nguvu’ yake yote licha ya wito wa kusitisha mapigano

‘Hakuna sehemu nchini Iran’ ambayo Israel haiwezi kufika – Netanyahu auambia Umoja wa Mataifa

f

Netanyahu anarejelea tena “laana ya Oktoba 7” ambayo anasema ilianza wakati Hamas ilipovamia lakini, ameongeza kuwa, “haikuishia hapo”.

Amesema kuwa tarehe 8 Oktoba, Hezbollah ilishambulia Israeli kutoka Lebanon na tangu wakati huo imerusha zaidi ya roketi 8,000.

Ameorodhesha wengine ambao wameishambulia Israeli ikiwa ni pamoja na Wahouthi wa Yemeni na kusema kwamba Aprili iliyopita, Iran iliishambulia moja kwa moja Israeli kutoka kwenye ardhi yake.

Anasema “hakuna mahali nchini Iran” ambapo “mkono mrefu” wa Israeli hauwezi kufikia, na “hiyo kwa Mashariki ya Kati yote”.

Ameongeza pia kwamba: “Mbali na kuwa wanakondoo wanaoongozwa kwenye machinjo, askari wa Israeli wamepigana kwa ujasiri wa ajabu na kwa ushujaa, na nina ujumbe mwingine kwa mkusanyiko huu na kwa ulimwengu nje ya ukumbi huu – tunashinda.”

Unaweza pia kusoma zaidi kwingineko:

Mamlaka ya Lebanon yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja

Hakuna usitishaji vita, hakuna njia rahisi kwa Israel au Hezbollah

Israel yasema imeshambulia maeneo lengwa 75 ya Hezbollah usiku kucha

Vita inaweza tu kumalizika kwa kusambaratisha Hezbollah – waziri wa Israel

Israel yashambulia ‘ikijiandaa kwa uwezekano wa kuingia’ Lebanon – Mkuu wa jeshi

Hezbollah ina uwezekano wa kuwa na silaha nyingi

Kiongozi mkuu wa Iran asema ‘Hezbollah ni washindi’

Netanyahu: Israel ‘haitapumzika’ katika mashambulizi ya Hezbollah hadi raia wake warejee nyumbani

g

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa vita hivi vinaweza kumalizika sasa ikiwa Hamas itajisalimisha.

Lakini anaongeza kuwa Israel lazima pia iishinde Hezbollah nchini Lebanon.

Anasema siku moja baada ya mashambulizi ya Hamas, Hezbollah ilirusha makombora na kuwalazimisha zaidi ya Waisraeli 60,000 kaskazini mwa Israel kuondoka makwao.

“Inatosha – hatutapumzika hadi raia wetu warudi makwao.”

“Hatutakubali jeshi la kigaidi kwenye mpaka wetu wa kaskazini kutekeleza mauaji mengine ya mtindo wa Oktoba 7,” amesema.

Hezbollah ilirusha makombora na roketi kutoka kwenye shule, hospitali na nyumba za kibinafsi za raia wa Lebanon, amesema.

Anasema kuwa Israel “haiko vitani na watu wa Lebanon”, bali katika vita na Hezbollah ambayo “imeiteka nchi yako”. Israel haina chaguo na ina kila haki ya kuondoa tishio hili, anasema.

Netanyahu kuhusu Iran: Ukitupiga, tutakupiga

f

Netanyahu amesema Umoja wa Mataifa lazima “urejeshe” vikwazo dhidi ya Iran na “ni lazima sote tufanye kila tuwezalo kuhakikisha Iran haipati silaha za nyuklia”.

Akihutumia Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, Waziri huyo mkuu wa Israel amesema amekuwa akiionya dunia dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran, ambao anasema “imeuchelewesha” kwa takriban muongo mmoja lakini hajausimamisha.

“Kwa ajili ya amani na usalama wa dunia nzima, hatupaswi kuruhusu hilo kutokea,” anasema, akimaanisha Iran kupata silaha za nyuklia.

“Nina ujumbe kwa wadhalimu wa Tehran,” anaongeza. “Ukitupiga, tutakupiga.”

Awali alipoanza hotuba yake Netanyahu alisema kwamba “hakuwa na nia ya kuja” kwenye Baraza Kuu mwaka huu kwani nchi yake iko vitani “inapigania maisha yake”.

“Niliamua kuzungumza katika Umoja wa Mataifa baada ya ‘uongo’ kuhusu Israel,” asema

Hata hivyo, uamuzi wake wa kufanya hivyo ulifuatia kile alichokiita “uongo na kashfa” kuhusu nchi yake iliyosemwa na watu wengine waliosimama kwenye jukwaa, anasema.

Anaongeza kuwa anataka kuja na “kuweka rekodi” kwamba Israeli inatafuta amani.

Netanyahu alionyesha ramani huku akijaribu kutofautisha “baraka” ya maendeleo ya Israeli na “laana” ya ushawishi wa Iran katika eneo.

Uchokozi wa Iran utahatarisha kila nchi katika Mashariki ya Kati – na dunia nzima, Netanyahu ameuambia Umoja wa Mataifa.

“Iran inataka kulazimisha itikadi kali zaidi ya Mashariki ya Kati, na inatishia ulimwengu mzima.”

Ulimwengu umeituliza Iran, anasema, na kufumbia macho ukandamizaji wa ndani wa Iran na uchokozi wa nje.

Mwanaharakati ‘mgonjwa mahututi’ wa Ghana anyimwa dhamana

h
Maelezo ya picha,Oliver Barker-Vormawor kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya polisi

Mwanaharakati wa Ghana aliyezuiliwa ambaye alikuwa mwandalizi mkuu wa maandamano ya hivi majuzi ya kupinga uchimbaji madini amenyimwa dhamana pamoja na wengine 11, licha ya kuwa mgonjwa mahututi.

Oliver Barker Vormawor alifikishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kukana mashtaka mengi, yakiwemo kukusanyika kinyume cha sheria na kumshambulia afisa wa umma.

Bw Vormawor atazuiliwa na polisi kwa muda wa wiki mbili kisha afike mahakamani. Amekuwa akitibiwa katika hospitali ya polisi kwa ugonjwa ambao haukujulikana.

Mwanaharakati huyo ambaye ni mhitimu wa Cho kikuu cha Cambridge alipanga maandamano ya siku tatu kupinga hatua dhidi ya uchimbaji haramu wa madini, unaojulikana kwa kienyeji kama “galamsey”, ambao umelaumiwa kwa kuchafua 60% ya maji ya Ghana.

Putin achora mstari mwekundu wa nyuklia kwa nchi za Magharibi

g

Rais Vladimir Putin amechora “mstari mwekundu” kwa Marekani na washirika wake kwa kuashiria kwamba Moscow itafikiria kujibu silaha za nyuklia ikiwa watairuhusu Ukraine kushambulia ndani kabisa ya Urusi kwa makombora ya masafa marefu ya Magharibi. .

Lakini wengine katika nchi za Magharibi wanauliza: je, ni kweli anamaanisha hivyo?

Swali hili ni muhimu kujiuliza katika hali ya vita. Iwapo Putin anababaika, kama Ukraine na baadhi ya wafuasi wake wanavyoamini, basi nchi za Magharibi zinaweza kuhisi tayari kuongeza uungaji mkono wake wa kijeshi kwa Kyiv bila kujali vitisho vya Moscow.

Iwapo anamaanisha anachokisema kuna hatari, kama inavyosemwa mara kwa mara na Moscow pamoja na Washington, kwamba mzozo unaweza kugeuka kuwa Vita vya Tatu vya Dunia.

Katika matukio ya hivi punde ya ishara za onyo, Putin Jumatano aliongeza orodha ya matukio ambayo yanaweza kusababisha Urusi kutumia silaha za nyuklia.

Inaweza kufanya hivyo, alisema, kujibu shambulio kuu la kawaida la kuvuka mpaka lililohusisha ndege, makombora au ndege zisizo na rubani.

Shambulizi la Israel lawauwa wanajeshi 5 katika mpaka wa Syria na Lebanon

f
Maelezo ya picha,Wapiganaji wa Hezbollah wakionyesha baadhi ya silaha zao kwa vyombo vya habari

Wizara ya ulinzi ya Syria imesema katika taarifa yake kwamba wanajeshi watano wameuawa na wengine sita kujeruhiwa kufuatia shambulio lililotekelezwa na Israel.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa shambulio hilo lililotokea mapema asubuhi, lililengwa katika moja ya maeneo yao ya kijeshi katika mpaka wa Syria na Lebanon katika eneo la mashambani la Damascus.

Shambuli hili linadhaniwa kuwa ni sehemu ya mkakati wa Israel kukata kuzuia usambazaji wa silaha za Iran zinazotolewa kwa Hezbollah kupitia Syria.

Mapema wiki hii kamanda wa Jeshi la anga la Israel, Meja Jenerali Tomer Bar, alisema ingawa Israel imeharibu vibaya uwezo wa kijeshi wa Hezbollah, sasa inahitaji kusimamisha uwezo wa Hezbollah wa kuimarika tena. mfumo wa usamabazaji wa silaha kupitia Syria ni muhimu kwa hilo.

“Nchini Lebanon tutazuia uwezekano wowote wa upelekaji wa silaha nchini Lebanon kutoka Iran,” aliuambia mkutano wa maafisa siku ya Alhamisi.

Hezbollah inapata msaada mkubwa wa kijeshi na kifedha kutoka Iran na ni mshirika wa rais wa Syria Bashar al-Assad.

Ukraine yasema ndege zisizo na rubani 24 za Urusi zimedunguliwa huku moja ikiingia Romania

h

Urusi imeishambulia Ukraine kwa ndege 32 zisizo na rubani aina ya Shahed, pamoja na makombora mawili ya Kh-22 na kombora moja la balistiki la Iskander-M, jeshi la anga la Ukraine liliripoti.

Kulingana na ripoti ya asubuhi, ndege 24 kati ya 32 za kamikaze zilidunguliwa.

Jeshi la anga linasema ndege moja isiyo na rubani iliingia kwenye anga ya Romania na nyingine “ilitoweka ndani.”

Romania imekiri ukiukaji wa anga lake wa ndege ya Urusi isiyo na rubani.

Ndege isiyo na rubani ya Urusi huenda ilikiuka anga ya Romania kwa “kipindi kifupi sana”, “chini ya dakika tatu” Ijumaa usiku wakati wa shambulio dhidi ya nchi jirani ya Ukraine, wizara ya ulinzi ya Romania ilisema.

Kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye mji wa Izmail katika mkoa wa Odessa, ulio kwenye mpaka na Romania kwenye wa Danube, watu watatu waliuawa na 14 walijeruhiwa, ofisi ya mwendesha mashtaka wa mkoa wa Odessa ilisema Ijumaa. Jeshi la Urusi halikutoa maoni yoyote juu ya data hizi.

“Mfumo wa rada wa Romania umebainisha uwezekano kwamba moja ya ndege zisizo na rubani zilizohusika katika shambulio la Ukraine zilivuka anga ya Romania kwa muda mfupi sana – chini ya dakika tatu – katika eneo la mpaka,” wizara ya ulinzi ya Romania ilisema katika tangazo lake.

Romania (mwanachama wa NATO) ilichukua ndege zake mbili za kivita za F-16, pamoja na ndege mbili za Uhispania F-18, ambazo zinafanya kazi ya kushika doria katika anga ya nchi hiyo. Wakaazi wa kaunti ya kusin mashariki ya Romania ya Tulcea walitahadharishwa kuchukua kutafuta hifadhi kufuatia tukio hilo, shirika la habari la Reuters linasema.

Mamlaka katika eneo la Odessa hapo awali ziliripoti shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye mji wa Izmail, ulioko kwenye mpaka na Romania karibu nae neo la Danube, ambalo liliwauwa raia watatu na kujeruhi wengine 12.

Jeshi la Urusi halijatoa kauli yoyote kuhusu shambulio jipya la ndege zisizo na rubani dhidi ya Ukraine.

IDF yadai kuwaua viongozi wengine wakuu zaidi wa Hezbollah katika shambulizi lililopita

Jeshi la Israel linasema kuwa viongozi wakuu waandamizi wa Hezbollah waliuawa wakati wa mashambulizi katika eneo la Beirut siku ya Jumanne.

Katika operesheni waliyoiita “Mishale ya Kaskazini” IDF hapo awali ilisema ilimuua mkuu wa makombora na Kikosi cha Roketi cha Hezbollah – Ibrahim Muhammad Qabisi.

Katika taarifa zake za hivi punde jeshi la Israel linasema wakuu wengine wa kundi hilo waliuawa , akiwemo naibu wa Qabisi.

Wakati hayo yakijiri aubuhi ya leo zimeshuhudiwa picha zinazoonyesha makombora juu ya Haifa yakizuiwa.

Mfumo wa kupambana na makombora wa Iron Dome wa Israel ulikatiza safari za makombora juu ya Haifa, yaliyofyatuliwa kutoka Lebanon.

IDF inasema baadhi ya roketi zimeanguka katika maeneo ya wazi.

g
f
Reuters

Shambulizi laua wanafamilia tisa nchini Lebanon – ripoti

Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba shambulizi la usiku kucha la Israel limeua watu tisa, wakiwemo watoto wanne, wa familia moja.

Wakimnukuu Meya Mohammad Saab, Reuters inasema shambulizi hilo lilifanyika katika mji wa Shebaa kusini mwa Lebanon.

Hezbollah inasema ilirusha makombora hadi Tiberias na Haifa

Hezbollah imedai hivi punde kwamba ilishambulia maeneo mawili nchini Israel – Tiberias na Kiryat Ata huko Haifa.

Hapo awali tulikufahamisha kuhusu ving’ora vinavyolia katika maeneo hayo mawili ambayo yote yanapatikana kaskazini mwa Israel.

Kundi linaloungwa mkono na Iran linasema katika taarifa yake kwamba lililenga Tiberias “kwa wingi wa makombora”.

Mamlaka ya Lebanon yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja

.

Waziri wa mambo ya nje, Abdallah Bou Habib, amezungumza katika Umoja wa Mataifa na kusema nchi yake inavumilia mzozo unaotishia uwepo wake, na kwamba ilikuwa ni muhimu kuukomesha kabla haujafikia hatua ya kutozuilika.

Hezbollah pia imeashiria kuwa haiko tayari kurudi nyuma, na inaendelea kurusha makombora dhidi ya Israel.

Upande mwingine, Israel imesema itaendelea kuwalenga Hezbollah huku mazungumzo yakiendelea, katika mashambulizi ambayo tayari yameua mamia ya watu kote Lebanon na kuwalazimisha makumi ya maelfu kuyahama makazi yao.

Huku kukiwa na shinikizo kubwa hospitalini na idadi inayoongezeka ya wakazi waliokimbia makazi yao, mamlaka ya Lebanon inaomba kusitishwa kwa mapigano mara moja.

Mazungumzo ya kusitisha mapigano yataendelea hata kama mapigano yanaendelea – Netanyahu

.

Mapema leo asubuhi, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel ilitoa taarifa ikitaka “kufafanua mambo machache” kuhusu kile ilichokiita “taarifa nyingi potofu kuhusu mpango wa kusitisha mapigano unaoongozwa na Marekani”.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Israel “iko pamoja na malengo ya mpango unaoongozwa na Marekani wa kuwawezesha watu walio kwenye mpaka wetu wa kaskazini kurejea salama kwenye makazi yao”.

Inaongeza kuwa timu zilikutana Alhamisi, na inasema majadiliano yataendelezwa katika siku zijazo.

Kauli hiyo inafuatia washirika wakiwemo Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika kipindi cha siku 21 “ili kutoa nafasi kwa diplomasia kuelekea kukamilika kwa suluhu la kidiplomasia” na kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.

Kufikia Alhamisi, pendekezo hilo lilikuwa limekataliwa na wanasiasa wa Israel akiwemo waziri wa mambo ya nje Israel Katz ambaye alisema “hakutakuwa na usitishaji mapigano kaskazini”.

Ikulu ya White House baadaye ilisema pendekezo la kusitisha mapigano “limeratibiwa” na Israel, licha ya madai ya Netanyahu.

Jeshi la Israel lasema limenasa kombora lililorushwa kutoka Yemen

Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa limefanikiwa kunasa kombora lililorushwa kutoka Yemen, baada ya ving’ora vya mashambulizi ya anga kusikika katikati mwa Israel.

Makundi ya Houthi ya Yemen mara kwa mara yamekuwa yakirusha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea Israel tangu vita vya Gaza kuanza.

Mengi yamenaswa, lakini mtu mmoja aliuawa mwezi Julai baada ya ndege isiyo na rubani kushambulia Tel Aviv, na kombora kutua katika eneo lisilo na watu katikati mwa Israel mapema mwezi huu.

Waasi wa Houthi, wanaoungwa mkono na Iran, hawajatoa maoni yoyote kuhusu uvamizi wa kombora usiku wa kuamkia leo.

Alabama yatekeleza hukumu ya kifo ya pili ya gesi ya nitrojeni Marekani

.

Jimbo la Marekani la Alabama limetekeleza hukumu ya kifo kwa Alan Eugene Miller – Mmarekani wa pili kuwahi kuuawa kwa kuvuta gesi ya nitrojeni.

Miller, mwenye umri wa miaka 59, alihukumiwa kifo kutokana na mauaji ya Lee Holdbrooks, Christopher Scott Yancy na Terry Lee Jarvis mnamo mwaka 1999.

Hukumu ya kifo kwake ni ya tano nchini Marekani ndani ya kipindi cha wiki moja – matumizi makubwa zaidi ya adhabu ya kifo katika zaidi ya miongo miwili.

Pia mnamo Alhamisi, Emmanuel Littlejohn alidungwa sindano ya sumu huko Oklahoma baada ya gavana wa jimbo hilo kukataa ombi la kuhurumiwa la dakika ya mwisho.

Mauaji ya Miller ni ya 18 hadi sasa mwaka huu – na wengine saba wamepangwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyosalia ya 2024.

Pia ni adhabu ya 1,600 ya kifo nchini Marekani tangu mahakama ya juu zaidi ya taifa hilo kurejesha hukumu ya kifo mnamo 1976.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment