Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Jeshi la Israeli limeripotiwa kutekeleza mashambulio ya anga katika ngome za wapiganaji wa RSF mjini Khartoum kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwenye jeshi na watu walioshuhudia.

Makabiliano hayo yameripotiwa kuanza mapema siku ya Alhamis, hii ikielezwa kuwa mojawapo na oparesheni kubwa na ya kwanza ya jeshi la Sudan baada ya miezi kadhaa dhidi ya RSF.
Jeshi la Sudan limekuwa likipambana kudhibiti tena maeneo ya mji mkuu wa Khartoum yanayodhibitiwa na RSF.
Chanzo cha kijeshi kimeliambia shirika la habari la AFP kwa maofisa wa jeshi la serikali walikuwa wanapigana na waasi katika mji mkuu, kwa maana ya RSF.

Kwa mujibu wa chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa, wanajeshi wa serikali walikuwa wamevuka vivukio vitatau muhimu ambavyo vilikuwa chini ya udhibiti wa RSF.
Tangu mapigano kuzuka mwezi April mwaka wa 2023, kati ya vikosi tiifu kwa mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na vile vya aliyekuwa naibu wake Mohamed Hamdan Daglo, RSF ilikuwa imefanikiwa kuwaondoa wanajeshi wa serikali kutoka katika mji wa Khartoum.
Mwezi Februari mwaka huu, jeshi lilikuwa limefanikiwa kudhibiti mji wa Omdurman, ambayo ni sehemu ya mji mkuu Khartoum.

Wakaazi katika mji wa Omdurman wameripoti kuwepo kwa makabiliano, mabomu yakielezwa kuanguka katika majengo ya watu, ndege za kijeshi zikionekana kupaa juu ya makaazi hayo ya raia.
Makabiliano kati ya pande hizo hasimu yamekuwa yakishuhudiwa katika maeneo ya watu wengi.
Inakadiriwa kwamba kati ya watu Elfu 20,000 hadi 150,000 wameuawa katika vita hivyo wakati wengine waliofariki, takwimu zao zikikosa kufahamika.
Zaidi ya watu Milioni 10 wamepoteza makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.