MAMBO 7 Makubwa YANAYOWAFELISHA

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wengi Wanapo JIAJIRI…

i. Kufanya Mambo Mengi kwa Wakati Mmoja

ii. Tamaa ya Kupanuka kwa Haraka

iii. Kutumia Pesa Mahali Palipo na Tija Ndogo

iv. Kukosa Nidhamu ya Muda

v. Kukosa Mpango Wa Biashara

vi. Kukosa Ujuzi wa Kuuza

vii. Kuridhika Mapema Sana

Leo katika makala hii tutaangalia jambo la nne.

– Kukosa Nidhamu ya Muda.

Moja ya sentensi hatari sana watu huwa wanaisema wanapoanza kujiajiri ni…

“Siku hizi hakuna mtu wa kunipelekesha…

…huwa naamua mwenyewe niingie saa ngapi ofisini na nitoke saa ngapi”.

Ninawafahamu watu wengi sana ambao walipokuwa wameajiriwa walikuwa ni wafanyakazi wazuri.

Tena waliotegemewa na kusifiwa na ofisi nzima, ila walipoenda kujiajiri WALIFELI.

Moja ya sababu kubwa sana ilikuwa ni kukosa nidhamu ya muda.

Hatari mojawapo ya kujiajiri mwenyewe ni kuwa unatakiwa kujisimamia wewe mwenyewe.

Watu wengi sana hawana uwezo wa kujisimamia wenyewe hasa kwenye muda.

Hii ndio maana wakisimamiwa chini ya ajira huwa wanafanya vizuri.

Ila wanapoamua kujisimamia wenyewe huwa hawafanyi vizuri kabisa.

Watu wengi sana wanapojiajri huwa wanatumia muda wao vibaya kwa sababu hakuna mtu wa kuwasimamia.

Au wa kuwakemea wanapochelewa kuingia au kutoka ofisini.

Hii inamaanisha, wengi wanaoamua kujiajiri huwa wanapoteza muda mwingi sana.

Na hii huwapunguzia matokeo wanayopata.

Kama haujaweza kujenga nidhamu ya muda kabla haujajiajiri…

…hii itakuwa ni kikwazo kikubwa sana kwako pale utakapoamua kujiajiri mwenyewe.

Kumbuka unahitaji nidhamu ya hali ya juu zaidi unapojiajiri zaidi ya hata unapokuwa umeajiriwa…

…kwa sababu kwenye kujiajiri hakuna wa kukushurutisha.

Ukihitaji kujifunza kwa kina MAMBO 7 Makubwa YANAYOWAFELISHA Wengi Wanapo JIAJIRI…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment