DRC: HRW yashutumu RDF na M23 kwa ‘kushambulia’ kambi za watu waliokimbia makazi yao

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch linashutumu jeshi la Rwanda (RDF) na kundi lenye silaha la M23 kwa “kushambulia kwa mabomu” kambi za watu waliokimbia makazi yao karibu na Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kambi za watu waliohama makazi yao huko Goma, Mei 6, 2024.
Kambi za watu waliohama makazi yao huko Goma, Mei 6, 2024. © AUBIN MUKONI / AFP

Tangu M23 kuchukuwa udhibiti wa mji wa Saké na kukaribia uwanja wa vita wa Goma mwanzoni mwa mwaka, angalau mara tano, mabomu na roketi vimerushwa kuelekea kambi za wakimbizi wa ndani au maeneo yenye wakazi wengi karibu na Goma, kulingana na Human Right Watch.

Mnamo Mei 3, “kati ya saa 4 na saa 5 mchana.,” kulingana na Human Rights Watch, “angalau roketi tatu” zilirushwa katika kambi za wakimbizi wa ndani kilomita 15 magharibi mwa Goma. Roktei hizo zilikuja, linasema shirika hilo, kutoka ngome ya jeshi la Rwanda na M23 kaskazini magharibi mwa Saké, nchini DRC. Siku hiyo, raia 17 waliuawa, ikiwa ni pamoja na watoto 15.

Wiki chache mapema, Februari 2, roketi iliyohusishwa na vikosi vya Rwanda na M23 ilianguka chini ya mita 100 kutoka shule ya msingi, tunaweza kusoma katika ripoti hii ambayo inaandika “uhalifu wa kivita” na kukemea “kutojali kabisa kwa maisha ya raia” kwa upande wa pande zote katika mzozo huo. Katika visa vyote viwili, ni “roketi za milimita 122”, silaha nzito za milipuko zinazojulikana kuwa zisizo sahihi ndizo zilirushwa.

“Ukiukaji wa sheria za vita”

Kushambulia maeneo yenye wakazi wengi bila kutofautisha kwa uwazi smaeneo ya kiraia na kijeshi ni “ukiukaji wa sheria za vita”, linakumbusha shirika la Human Rights Watch huku pia likionyesha wajibu wa jeshi la Kongo ambalo, kwa kuweka silaha zake karibu na kambi, huwaweka raia katika mazingira mazito ya kushambuliwa kwa ulipizaji kisasi.

Hili ni tukio lililotokea hasa, kulingana na HRW, Mei 31 wakati jeshi la Kongo lilipoanza kufyatua risasi kutoka eneo lililopo mita mia chache kutoka kituo cha kulelea watoto katika kambi ya Lushagala, na hivyo kuacha muda kwa wafanyakazi kuhama kabla ya majibu. “Roketi” ilianguka “mita 100 kutoka kituo cha watoto,” kulingana na Human Rights Watch.

Ripoti hiyo pia inabaini mfululizo mrefu wa dhuluma zinazohusishwa na jeshi la Kongo na wanamgambo wa Wazalendo ndani ya kambi za watu waliokimbia makazi yao: mauaji, mateso, mauaji ya watu wanaoshikiliwa na idara za usalama na kesi nyingi za ubakaji.

Mwezi Agosti, Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) lilisema kuwa zaidi ya mwanamke mmoja kati ya 10 katika kambi ndani na karibu na Goma waliripoti kubakwa kati ya mwezi wa Novemba 2023 na mwezi wa Aprili 2024, huku idadi hiyo ikiongezeka hadi 17% katika baadhi ya kambi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment