Aina mpya ya ‘Papa zimwi’ yagunduliwa katika maji ya New Zealand

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

.

Wanasayansi wa New Zealand wamegundua aina mpya ya “Papa zimwi” – aina adimu ya samaki ambao ni vigumu sana kuwaona kwa sababu wanaishi kwenye kina kirefu katika Bahari ya Pasifiki.

Pia anajulikana kama spookfish au chimera, na wana uhusiano wa karibu na papa wa kawaida na samaki wa Ray fish. Hawana magamba na mifupa yao imetengenezwa kwa katileji kabisa.

Dk Brit Finucci, mmoja wa wanasayansi waliogundua samaki aina ya Australasian Narrow-nosed Spookfish, alisema ugunduzi huo ulikuwa “wa kusisimua”.

“Makazi yao yanawafanya kuwa wagumu kusoma na kufuatilia, ikimaanisha kuwa hatujui mengi kuhusu biolojia yao au hali ya tishio,” alisema.

Dk Finucci na watafiti wengine kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Maji na Utafiti wa Anga ya New Zealand (Niwa) walimpata kiumbe huyo katika eneo la sakafu ya bahari linalojulikana kama Chatham Rise, ambalo liko mashariki mwa New Zealand.

Papa zimwi kwa kawaida huishi kwenye kina cha hadi 2,600m (maili 1.6).

Dk Finucci alisema spishi hiyo ilitofautishwa na pua yake ndefu isiyo ya kawaida, ambayo inaweza kusheheni nusu ya urefu wa mwili wake.

Amempa samaki huyo mpya jina la kisayansi: Harriota avia.

“Avia inamaanisha nyanya kwa Kilatini, nilitaka kumpa taadhima hii kwa sababu aliniunga mkono kwa fahari kupitia kazi yangu kama mwanasayansi,” Dk Finucci alielezea.

Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yanasababisha ‘mauaji ya watu wengi’ waziri wa afya asema

.

Waziri wa afya wa Lebanon amesema kinachoendelea nchini mwake ni “mauaji”, huku hospitali zikijitahidi kukabiliana na idadi ya waliopoteza maisha kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel yaliyoenea kwa siku mbili yakilenga kundi la Hezbollah.

Dkt Firass Abiad aliiambia BBC ni “wazi” kwamba wengi wa watu 550 waliouawa katika mashambulizi ya Jumatatu walikuwa raia, ikiwa ni pamoja na watoto na wanawake.

Israel ilisema ilishambulia mamia ya maeneo ya Hezbollah, ikilishutumu kundi hilo kwa kuficha silaha katika maeneo ya makazi.

Siku ya Jumanne, jeshi la Israel lilimuua mkuu wa vikosi vya roketi vya Hezbollah wakati mashambulio hayo yakiendelea, huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akisema kundi hilo lilikuwa linaiongoza Lebanon “kuzimu”.

Hezbollah ilijibu kwa kurusha zaidi ya roketi 300 kaskazini mwa Israel, na kujeruhi watu sita, kulingana na jeshi.

Ijapokuwa hakuna upande ulionekana kuwa na nia ya kurudi nyuma, Rais wa Marekani Joe Biden aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba mzozo kamili “haukuwa wa maslahi ya mtu yeyote” na kusisitiza kwamba “suluhisho la kidiplomasia bado linawezekana”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alionya kwamba ulimwengu “hauwezi kumudu Lebanon kuwa Gaza nyingine”.

Takriban mwaka mmoja wa mapigano ya kuvuka mpaka kati ya Israel na Hezbollah yaliyochochewa na vita huko Gaza, yameua mamia ya watu wengi wao wakiwa wapiganaji wa Hezbollah, na maelfu ya wengine kuyahama makazi yao pande zote mbili za mpaka huo.

Hezbollah imesema inaiunga mkono Hamas na haitakoma hadi kutakapokuwa na usitishaji vita huko Gaza.

Makundi yote mawili yanaungwa mkono na Iran na yamepigwa marufuku kuwa mashirika ya kigaidi na Israel, Uingereza na nchi nyinginezo.

Kesi ya 11 dhidi ya Sean ‘Diddy’ Combs yawasilishwa akiwa bado gerezani

.

Mwanamuziki wa Hip-hop Sean “Diddy” Combs kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa serikali akisubiri kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ulaghai na utumwa wa ngono.

Kukamatwa kwake wiki iliyopita mjini New York kulitokea huku kukiwa na msururu wa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa kimwili, dhidi yake na mengine yakianzia miaka ya 1990.

Mlalamishi wa 11 na wa hivi punde kujitokeza ni Thalia Graves, anadai Combs na mlinzi wake walimpa dawa za kulevya , kumfunga na kumbaka mnamo 2001, na kurekodi tukio hilo.

Rapa huyo mzaliwa wa Harlem amekana makosa ya jinai.

Kesi ya jinai inahusu nini?

Combs, 54, alikamatwa Jumatatu Septemba 16 katika hoteli ya New York kwa tuhuma za kula njama, kuendesha biashara ya utumwa wa ngono na uhalifu mwingine .

Waendesha mashtaka wa serikali kuu wamemshutumu kwa “kuunda biashara ya uhalifu” ambapo “aliwanyanyasa, kutishia, na kulazimisha wanawake na wengine walio karibu naye kutimiza tamaa zake za kingono, kulinda sifa yake, na kuficha tabia yake”.

Walisema Combs ametumia dawa za kulevya, vurugu na nguvu ya hadhi yake “kuwavutia waathiriwa wa kike” katika vitendo vya ngono katika karamu zake zinazoitwa “Freak Offs”.

Pia walifichua walikuwa wamepata bunduki, risasi na chupa zaidi ya 1,000 za mafuta wakati wa uvamizi katika nyumba za Combs huko Miami na Los Angeles mnamo Machi.

Trump aonywa na huduma za usalama Marekani juu ya vitisho vya mauaji ya Iran – kambi yake ya kampeni

.

Donald Trump amefahamishwa na idara ya kijasusi ya Marekani kuhusu vitisho kutoka kwa Iran vya kutaka kumuua, kambi yake ya kampeni ilisema.

Mgombea urais wa chama cha Republican alifahamishwa “kuhusu vitisho vya kweli na mahususi kutoka kwa Iran vya kutaka kumuua katika juhudi za kuyumbisha na kuzusha machafuko nchini Marekani”, kambi yake ya kampeni ilisema katika taarifa.

Haikufafanua madai hayo, na haikufahamika mara moja iwapo vitisho iliyokuwa inarejelea ni vipya au viliripotiwa awali.

Serikali ya Iran haikujibu mara moja ombi la maoni yake, lakini Tehran hapo awali ilikanusha madai ya Marekani ya kuingilia masuala ya Marekani.

“Maafisa wa ujasusi wamegundua kuwa mashambulizi haya yanayoendelea na yaliyoratibiwa yameongezeka katika miezi michache iliyopita,” mkurugenzi wa mawasiliano wa kambi ya kampeni ya Trump, Steven Cheung alisema katika taarifa hiyo.

“Maafisa wa utekelezaji wa sheria katika mashirika yote wanafanya kazi kuhakikisha Rais Trump analindwa na uchaguzi hauingiliwi,” aliongeza.

BBC imeenda kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa nchini Marekani kwa maoni.

Haya yanawadia baada ya Bw Trump kunusurika katika jaribio la mauaji mnamo Julai 13, alipojeruhiwa na mtu mwingine kuuawa kwa kupigwa risasi kwenye mkutano huko Pennsylvania.

Nia ya tukio hilo bado haijabainika na bado linachunguzwa.

Siku chache baadaye, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba maafisa walipokea taarifa za kijasusi kuhusu njama zinazodaiwa kuwa za Iran dhidi ya rais huyo wa zamani.

Maafisa wa Iran wakati huo walikanusha madai hayo na kusema ni ya “uovu”, iliripoti mshirika wa BBC wa Marekani CBS habari.

“Iwapo ‘watamuua Rais Trump,’ jambo ambalo linawezekana, ninatumai kuwa Marekani itaiangamiza Iran, kuifuta kabisa kwenye uso wa Dunia – Ikiwa hilo halitafanyika, Viongozi wa Marekani watachukuliwa kuwa waoga ‘wasio na ujasiri’!” Bw Trump aliandika kwenye jukwaa lake la Truth Social platform wakati huo.

Kisha tarehe 15 Septemba, Shirika Maalum la Usalama liliona bunduki ikipenya kwenye uzio katika Klabu ya Gofu ya Kimataifa ya Trump huko West Palm Beach.

Ofisa wa shirika hilo alifyatua risasi Bw Trump alipokuwa akicheza gofu.

Ryan Routh ashtakiwa kwa jaribio la kumuua Trump

.

Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka mwanamume aliyekamatwa karibu na uwanja wa gofu wa Donald Trump wa Florida kwa jaribio la kumuua mgombeaji urais.

Hili linawadia siku moja baada ya jalada la mahakama kuonyesha Ryan Wesley Routh alikuwa ameandika barua miezi kadhaa iliyopita akisema alikusudia kumuua Trump.

Routh, 58, tayari anakabiliwa na hadi miaka 20 jela kwa mashtaka mawili yanayohusiana na bunduki.

Lakini anakabiliwa na kifungo cha juu zaidi cha maisha jela ikiwa atapatikana na hatia kwa mashtaka mapya na makubwa zaidi.

“Vurugu zinazolenga maafisa wa umma zinahatarisha kila kitu ambacho nchi yetu inasimamia,” Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland alisema katika taarifa, akiapa “kutumia kila chombo kilichopo” kumuwajibisha Routh.

Trump ameishutumu serikali kwa kushughulikia kesi hiyo vibaya, akiandika katika ujumbe wa mtandao wa kijamii siku ya Jumatatu kwamba wizara ya sheria inapaswa “KUACHA FLORIDA ISHUGHULIKIE KESI HIYO!”

Lakini Garland alikataa hilo, akiwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne kwamba shirika lake “litatafuta kushirikiana na kupata usaidizi kutoka kwa” maafisa wa serikali “kulingana na sheria”.

Nyaraka za mahakama zinaonyesha kesi hiyo imetolewa bila kufuata mpango maalumu kwa Jaji wa Wilaya ya Marekani Aileen Cannon.

Bi Cannon ndiye jaji wa Florida Kusini ambaye alipewa kesi ya hati za siri za serikali ya Trump mwaka jana na ambaye aliitupilia mbali mapema mwaka huu. Uamuzi wake kwa sasa uko chini ya rufaa.

Jaji tofauti mnamo siku ya Jumatatu aliamuru Routh abaki rumande baada ya waendesha mashtaka kuhoji kuwa alikuwa na uwezekano wa kutoroka nchi na hatari kwa jamii.

Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha kizuizini huko Florida Kusini tangu kukamatwa kwake tarehe 15 Septemba.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment