Wahamiaji wanaoingia nchini Uingereza kwa kutumia boti ndogo wafikia Elfu 25

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Idadi ya wahamiaji wanaoingia Uingereza kupitia eneo maarufu la bahari kwa kutumia boti ndogo imefikia elfu 25, hii ikiwa ni tangu mwanzoni mwa mwaka huu, takwimu za serikali zimeonesha.

Serikali imeahidi kuwa katika kipindi cha miezi 6 ijayo, inatarajia kuwarudisha kwenye nchi zao maelfu ya wahamiaji waliongia kinyume cha sheria.
Serikali imeahidi kuwa katika kipindi cha miezi 6 ijayo, inatarajia kuwarudisha kwenye nchi zao maelfu ya wahamiaji waliongia kinyume cha sheria. AFP – BEN STANSALL

Takwimu hizi zimetolewa wakati huu utawala wa chama cha Labour kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake chama cha Conservative, unahanhgaika kudhibiti wimbi la wahamiaji wanaotumia njia kati yake na Ufaransa.

Jumapili iliyopita wahamiaji zaidi ya 700 waliiingia nchini humo kutokea Ufaransa na kufanya idadi yao kufikia elfu 25 ndani yam waka huu pekee.

Serikali ya Uingereza ilikuwa imeingia kwenye makubaliano na nchi ya Rwanda kuhusu suala la wahamiaji.
Serikali ya Uingereza ilikuwa imeingia kwenye makubaliano na nchi ya Rwanda kuhusu suala la wahamiaji. © AFP – Ben Stansall

Mpango wa kukabiliana na wimbi la wahamiaji ulikuwa ni ajenda kubwa ya uchaguzi mkuu wa mwezi Julai, chama cha Labour kikiahidi kuja na mkakati mbadala badala ya ule wa kubadilishana wahamiaji na Rwanda ambao ulikosolewa na jumuiya ya kimataifa.

Serikali imeahidi kuwa katika kipindi cha miezi 6 ijayo, inatarajia kuwarudisha kwenye nchi zao maelfu ya wahamiaji waliongia kinyume cha sheria.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment