Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Yaani, kila unayemuona amefika mbali kwenye maisha yake, kuna wakati alitamani kuishia njiani.
Kwanza lazima kuna watu watakukataa.
Hata uwe unafanya kitu kizuri namna gani, kuna aina fulani ya watu kwa sababu wanazozijua wenyewe, watakukataa.
Kumbuka hili, sio lazima muwe mmegombana au uwe umewafanyia kitu kibaya.
Kuna wengine, watakukataa hata kama utawaonesha upendo.
Ndio maisha yalivyo, Kubali tu.
Ila Usisahau pia, utaona hali ya kuchelewa.
Yaani, utaona kama vile muda unaenda na mambo hayaendi haraka Kama inavyotamani.
Ukipiga Mahesabu yako unaona kama unatakiwa uwe umefika “level” Fulani
Au uwe unamiliki kitu Fulani, Ila haiko hivyo.
Usikate tamaa kwa kuhisi kuwa umechelewa, ni msimu ambao lazima uupitie katika kuelekea maono yako.
Nakuombea ili leo upate nguvu za ziada ili leo uchukue hatua moja zaidi hata kama unaona nguvu zimekuishia.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.