Israeli yaendelea kurusha makombora nchini Lebanon, zaidi ya watu 450 wakiuuawa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore

Mashambulio ya Israeli nchini Lebanon yaliyolenga kundi la Hezbollah, yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 490 huku wengine zaidi ya 1500 wakijeruhiwa.

Wito umetolewa kwa pande hasimu kuepuka vitendo vinavyoweza kuchochea mzozo mkubwa mashariki ya kati.
Wito umetolewa kwa pande hasimu kuepuka vitendo vinavyoweza kuchochea mzozo mkubwa mashariki ya kati. REUTERS – Aziz Taher

Haya ndio mauaji makubwa kuwahi kutokea kwa siku moja nchini Lebanon, baada ya miaka ishirini, ambayo pia yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao.

Jeshi la Israeli linasema, limeshambulia ngome 1,300 Hezbollah na kuharibu miundombinu ambayo kundi hilo linaloungwa mkono kundi la Hamas limekua likitumia tangu vita vya 2006. Daniel Hagari, ni msemaji wa Jeshi al Israel.

“Kwa zaidi ya miaka 20, Hezbollah imetuma wapiganaji wake ndani ya makazi, na kutumia miundombinu ya kiraia, kutokana na hilo, kundi hili la kigaidi limeigeuza eneo la Kusini mwa Lebabon kuwa uwanja wa mapambano.”  AlisemaDaniel Hagari, msemaji wa Jeshi al Israel.

Waziri Mkuu wa Israeli katika ujumbe wa video amewaambia raia wa Lebanon kwamba nchi yake inawakabili wapiganaji wa Hezbollah na wala sio raia wa kawaida.
Waziri Mkuu wa Israeli katika ujumbe wa video amewaambia raia wa Lebanon kwamba nchi yake inawakabili wapiganaji wa Hezbollah na wala sio raia wa kawaida. AP – Hussein Malla

Katika hatua nyingine, Josep Borrel, mkuu wa será za kigeni wa umoja wa Ulaya amesema mzozo kati ya Israeli na Hezbollah unakaribia kuwa vita kamili.

“Kuendelea kwa mzozo huu ni hatari sana na unatia wasiwasi, naweza kusema kuwa tunakaribia kushuhudia vita kamili.” AmeelezaJosep Borrel, mkuu wa será za kigeni wa umoja wa Ulaya

Jumuiya ya kimataifa imeonekana kutilia shaka mashambulio ya Israeli nchini Lebanon, Marekani ikisema itatuma vikosi zaidi eneo la mashariki ya kati huku Ufaransa nayo ikiitisha kikao cha dharurua cha baraza la usalama la umoja wa mataifa kujadili mzozo huo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment