Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, upinzani unashinikiza kuachiwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa, na umeandaa maandamano siku ya Jumatano kupaza sauti zaidi.

Wanasiasa wa upinzani wanataka watu wote waliofungwa kwa sababu za kisiasa tangu rais Felix Tshisekedi alipoingia madarakani, waachiwe huru.
Siku ya Jumanne wanasiasa hao wakiongozwa na Moise Katumbi, wanatarajiwa kukutana kutoa maelezo ya kina kuhusu mpango wao wa maandamano.
Katumbi amesema hali imekuwa mbaya kwa sababu wapinzani na wanaharakati kutoka mashirika ya kiraia, wameendelea kukamtwa, kuzuiwa na kusumbuliwa na serikali iliyopo madarakani.

Miongoni mwa watu ambao upinzani unataka waachiwe huru ni Seth Kikuni ambaye amekuwa akizuiwa kwa wiki tatu sasa, lakini wanaendelea kudai haki baada ya kuuawa kwa Cherubin Okende na wapinzani waliozuiwa kwenye Gereza la Makala na wengine wao kudaiwa kubakwa.
Haya yanajiri wakati huu, rais Tshisekedi akiwa jijini New York anakotafuta uungwaji mkono wa nchi yake kuwa mwanachama wa Tume ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.