Burkina Faso: Jeshi linasema limezima majaribio kadhaa ya mapinduzi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore

Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imesema imefanikiwa kuzuia majaribio kadhaa ya mapinduzi yaliokuwa yamepangwa na afisa wa juu wa jeshi.

Paul-Henri Sandaogo Damiba na kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa sasa wa Burkina Faso.
Paul-Henri Sandaogo Damiba na kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa sasa wa Burkina Faso. © Photos AFP – Montage RFI

Hili limethibitishwa na Waziri wa usalama, ambaye amemtaja aliyewahi kuwa kiongozi wa kijeshi Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, kuhusika, huku washukiwa wengine wakikamatwa.

Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, aliondolewa madarakani mwaka wa 2022.

Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, Tarehe 3 Oktoba 2022 jijini  Ouagadougou.
Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, Tarehe 3 Oktoba 2022 jijini Ouagadougou. © Capture d’écran Facebook / Paul-Henri Sandaogo Damiba

Miongoni mwa watu wengine wanaozuiliwa kwa kuhusika na jaribio hilo ni pamoja na Ahmed Kinda, kamanda wa zamani wa kitengo maalum cha jeshi.

Damiba alichukua madaraka mwezi Januari mwaka wa 2022 baada ya kuangusha utawala wa aliyekuwa rais Roch Marc Christian Kabore.

Roch Marc Christian Kabore aliyekuwa rais wa Burkina Faso.
Roch Marc Christian Kabore aliyekuwa rais wa Burkina Faso. AP – Ludovic Marin

Baada ya miezi minane madarakani, Damiba aliondolewa na kapteni Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 34 ambaye kwa sasa ndiye rais wa kijeshi.

Chini ya utawala wa Traore, Burkina Faso imekatisha uhusiano wake na mkoloni wake wa zamani nchi ya Ufaransa na kuonekana kuegemea upande wa Urusi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment