VITA 5 Kubwa AMBAZO Kila MKOMBOZI Wa Familia LAZIMA AZISHINDE…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Uchungu Unaotokana na Utegemezi Wa Ndugu Wasio Na Shukrani.

ii. Ugomvi Usioisha Wewe Na Mwenzi Wako

iii. Kushindwa Kujiendeleza Kiuchumi

iv. Changamoto Ya Malezi Ya Watoto

v. Kupata Changamoto Za Kiafya

Leo katika makala hii tutaangalia vita ya kwanza:

– Uchungu Unaotokana na Utegemezi Wa Ndugu Wasio Na Shukrani.

Watu wengi wanaoinuliwa kama wakombozi kwenye familia zao huwa wanajitoa sana kwa ajili ya watu wengine.

Kwa sababu hii, huwa wanajikuta wanawekeza kila walichonacho katika kusaidia ndugu zao.

Hata hivyo baada ya muda huwa wanapitia katika hali ya uchungu sana wa nafsi zao kwa sababu…

…walewale ndugu ambao waliwasaidia na kujitolea sana kwa ajili yao, wanageuka kuwa sumu ya kuwalaumu sana.

Yani unakuta mtu maisha yake yote tangu aanze kupata pesa…

…amekuwa akizitumia kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya ndugu zake.

Lakini haishi kulaumiwa na kusemwa vibaya.

Kinachoumiza zaidi ni kuwa, unaweza kushindwa kufanya vitu fulani…

…kwa sababu ulitumia muda mwingi na rasilimali nyingi kuwasaidia watu wa familia yako.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment