Mbinu 10 Rahisi Za Kupata Mtaji Wa Biashara…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Nguvu Zako

ii. Ujuzi

iii. Msaada

iv. Mkopo

v. Kuuza Ulichonacho

vi. Mwekezaji

vii. Kuaminika

viii. Vikundi

ix. Akiba

x. Vifaa

Katika makala hii tutaangalia mbinu ya kumi VIFAA .

Jinsi Ya Kutumia VIFAA Ulivyonavyo Kama Mtaji Wa Biashara.

Kuna nini ulichonacho ambacho unaweza kuanza kukitumia kukupatia pesa ambazo zinaweza kukupa nguvu za kuanza kufanya biashara?

Kijana mmoja baada ya kunisikia nafundisha somo hili la MTAJI, akagundua kuwa anaweza kutumia TV yake kubwa kuanza kuonesha mechi za mpira wa miguu mtaani kwake. Akaanza kufanya hiyo biashara.

Binti mwingine aligundua ana vifaa vyote vinavyoweza kutengeneza vitafunwa “BITES” nzuri kwa sababu kwa kawaida anapenda kupika, akaanza kupika na kuviuza kwa majirani.

Je, wewe katika vitu ulivyonavyo kwa sasa, ni kitu gani ambacho kinaweza kuwa ni chanzo cha kukupa mtaji ambao unautaka?

Usisahau kuwa Mungu anapotaka kuwabariki watu huwa anawauliza “Wana Nini Mkononi?

Ukidharau kile kidogo ambacho Mungu amekupatia, unajifungia mlango wa kupata kikubwa unachokitafuta.

Ukihitaji kujifunza mbinu nyingine 9 za kupata Mtaji Wa biashara nashauri usome eBook MPYA ya MTAJI, Mbinu Rahisi Za Kupata Mtaji Wa Biashara.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment