Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. “Ningefanya Vitu Bila Kuogopa Changamoto Ambazo Zingetokea”.
ii. “Ningewekeza Muda Zaidi Katika Mambo Ambayo Ni Zaidi Ya Pesa Katika Maisha”.
iii. “Ningejifanyia Tathmini Za Kila Wakati”.
Leo katika makala hii tutaangalia majuto ya kwanza.
– Ningefanya Vitu Bila Kuogopa Changamoto Ambazo Zingetokea.
Mtaalamu nguli wa mambo ya kijamii Dr. Anthony Campolo aliwahi kufanya stadi ya kijamii (Sociological Study).
Stadi ambayo ilikuwa inalenga kutaka kujua watu wanapokuwa wazee sana huwa wanajutia mambo gani katika maisha yao.
Katika utafiti huo aliamua kuchukua wazee 50 ambao wote walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 95 na aliwauliza swali moja tu.
“Je, kama ungepewa nafasi ya kuishi tena ungefanya nini cha tofauti katika Maisha yako mapya”?
Ingawa yalipatikana majibu mengi sana kwa swali hili ila kuna majibu makubwa matatu ambayo yalijirudia sana katika majibu yote ambayo yalitolewa.
Cha kwanza kabisa ambacho wazee wengi wanasema wanajutia hawa walisema wangefanya kwa namna ya tofauti ni…
“Ningefanya vitu bila kuogopa changamoto ambazo zingetokea”
(I would risk more in my life).
Wengi wao walikiri kuwa ingawa wamefanikiwa kufanya mambo mengi na makubwa katika maisha yao…
…ila ukweli ni kuwa kama wangeishinda hofu ambayo ilikuwa inawakabili basi wangefika mbali sana.
Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyafanya ila hofu imekukamata na unaogopa kuchukua hatua.
Kumbuka kuwa maumivu ya kuikabili hofu yako leo ni madogo ukilinganisha na maumivu utakayoyapata utakapogundua hauna nguvu…
…muda na uwezo wa kufanya ambacho ulikuwa unakitamani kila siku.
Anza kuchukua hatua leo na ufanye unachotakiwa kufanya ili baadaye usijutie.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.