Lebanon: Raia wapokea ujumbe wa simu kutoka kwa Israel wakitakiwa kuondoka

Maofisa nchini Lebanon wameripoti kwamba raia nchini humo wanapokea ujumbe wa simu kutoka kwa Israeli ikiwaonya kuondoka, Ofisi wa Waziri wa mawasiliano Ziad Makary ikithibitisha kupokea moja ya ujumbe huo.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ofisi wa Waziri wa mawasiliano wa Lebanon Ziad Makary imethibitisha kupokea moja ya ujumbe huo.
Ofisi wa Waziri wa mawasiliano wa Lebanon Ziad Makary imethibitisha kupokea moja ya ujumbe huo. AFP – JOSEPH EID

Ripoti hii imekuja baada ya jeshi la Israeli kutoa taarifa kwa raia wa Lebanon kuondoka katika maeneo yanayoelezwa kwamba yanakaliwa na wapiganaji wa Hezbollah.

Israeli imeapa kutekeleza mashambulio mazito dhidi ya wapiganaji hao wa Hezbollah wanaouungwa mkono na Iran.

Wanajeshi wa Israeli wameripotiwa kutekeleza mashambulio mazito kusini mwa Lebanon
Wanajeshi wa Israeli wameripotiwa kutekeleza mashambulio mazito kusini mwa Lebanon AFP – JALAA MAREY

Hili limetajwa kuwa onyo la kwanza kutoka kwa Israeli kwa raia wa Lebanon tangu kuzuka kwa mapigano katika ukanda wa Gaza karibia mwaka mmoja uliopita.

Shirika la habari la kitaifa nchini Lebanon National News Agency (NNA) limeripoti kwamba raia kutoka katika maeneo ya Beirut pamoja na sehemu nyengine walikuwa wanapokea ujumbe huo wa onyo ambao umetoka kwa jeshi la Israeli wakitakiwa kuondoka kwa haraka.

Israeli inasema inawalenga wapiganaji wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran nchini Lebanon
Israeli inasema inawalenga wapiganaji wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran nchini Lebanon © AFP

Shirika hilo limeeleza kwamba ujumbe huu wa onyo ni mojawapo ya  vita vya kisaikolojia ambavyo Israeli inatumia.

Ofisi ya Makary iliokaribu na mji wa Beirut imethibitisha kupokea simu ambayo ilikuwa na ujumbe uliorekodiwa, ujumbe huo ukiwataka kuondoka kwenye jengo lao ilikuepuka kushambuliwa.

Watu wengine wemethibitisha kupokea ujumbe wa simu wenye onyo sawa na hilo kutoka kwa mtu ambaye nambari yake imefichwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment