Unapokuta na mtu asiyependa amani.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna wale watu ambao HAWATAKI AMANI na wewe.

Yaani, inawezekana mmegombana jambo fulani au umewakosea.

Ila walishaamua kuwa hawako tayari kuwa na amani na wewe.

Watu hawa ndani ya mioyo yao walishafanya maamuzi kuwa, kuwa na amani na wewe sio kipaumbele kwenye maisha yao.

Watu wa namna hii, utajitahidi sana KUJISHUSHA kwa kila namna.

Utajitahidi kufanya vitu ili uwaridhishe, Ila hawatakuwa tayari kuwa na Amani na wewe.

Kwa ufupi ni watu ambao wamechagua VITA na CHUKI kinyume nawe, maisha yao yote.

Hawa wanaweza kuwa sehemu ya familia yako, wanaweza kuwa ofisini au wakati mwingine ni mtu ambaye alikuwa ni Rafiki yako.

Kumbuka, katika mazingira Kama haya wajibu wako ni kufanya kile kilicho sahihi, Ila hautaweza kubadilisha moyo wa mtu kwa kile alichoamua.

Uwe makini, Kama umefanya kila kinachowezekana basi usilazimishe sana kwa sababu unaweza kupata madhara zaidi.

Watu wa hivi ni hadi wenyewe waamue kubadilika.

Usipoteze Furaha yako kwa ajili yao.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment