Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Uturuki itafanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na viongozi wa Somalia na Ethiopia, ikiwa ni katika juhudi za kupunguza mvutano kati yao kabla ya duru mpya ya mazungumzo yanayosimamiwa na Ankara, wizara ya mambo ya nje imethibitisha.

Uhusiano kati ya Mogadishu na Addis Ababa umeendelea kudorora tangu Ethiopia ilipoingia makubaliano yenye utata ya matumizi ya baharini ya eneo la Somalia lililojitenga, Somaliland mwezi Januari, mkataba huo ukiipa Ethiopia — moja ya nchi kubwa zaidi zisizo na bahari – kutumia bahari ya Somalia, kitendo ambacho Mogadishu inasema ni kuingiliwa kwa uhuru wake.
Awali Addis Ababa ilikuwa inatumia bandari ya Eritrea hadi pale nchi hizo mbili zilipoingia vitani kati ya mwaka 1998 na 2000 na tangu wakati huo, Ethiopia imekuwa ikipitisha bidhaa zake kupitia bandari ya Djibouti.

Uturuki, ambayo imekuwa ikifanya jitihada za diplomasia kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Ethiopia na Somalia tangu majira ya joto, ilifanya vikao viwili na pande hizo mwezi Julai na Agosti mwaka huu.
Duru ya tatu ya mazungumzo, ambayo yalipaswa kufanyika Jumanne ya wiki hii, yaliahirishwa huku waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Hakan Fidan akisema Ankara ingependa kukutana viongozi wa nchi hizo mbili kwa wakati tofauti kabla ya duru nyingine ya mazungumzo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.