Mwanaharakati aliyetekwa nyara Bob Njagi yuko hai – Rais wa wanasheria

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

  1. Mwanaharakati Bob Micheni Njagi na ndugu Jamil na Aslam Longton, ambao walikuwa wamebatizwa jina la Kitengela Watatu baada ya kutekwa nyara mwezi mmoja uliopita katika mji wa Kaunti ya Kajiado, wako hai.Watatu hao walisema waliachiliwa alfajiri ya Ijumaa, Septemba 20, saa chache baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuapishwa. Ndugu hao wa Longton walisema waliachiliwa na waliowateka na kuahidi kutoa taarifa zaidi kupitia kwa rais wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) Faith Odhiambo. Video iliyotumwa kwenye ukurasa wa X na Bi Odhiambo ilionesha kuwa ndugu hao wa Langton waliachiliwa mahali fulani huko Gachie na wakatembea hadi kwenye nyumba ambapo walidaiwa kuchaji simu zao za mkononi kabla ya kumpigia simu rais wa LSK.” Mnamo saa moja asubuhi Bob Njagi alifanikiwa kutafuta njia hadi kituo cha polisi cha Tigoni na kupata usaidizi. Yuko hai,” Bi Odhiambo alisema.”Kwa familia, marafiki na kila Mkenya ambaye ameendelea kuniombea, napenda kuthibitisha kuwa mimi ni mzima na pamoja na familia yangu. Sasa ni wakati wa kunyamazisha kelele, kushukuru kwa maisha na kila mtu atafakari kwa nini Kenya.Watatu hao waliotekwa nyara mnamo Agosti 19 huko Kitengela, waliachiliwa muda mfupi kabla ya Naibu Inspekta Jenerali Gilbert Masengeli kuashiria kwamba angefika kortini kuomba msamaha mahakamani na kueleza waliko.Bw. Masengeli alipatikana na hatia ya kudharau mahakama na Jaji Lawrence Mugambi na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.Mshirikishe mwenzako, Mwanaharakati aliyetekwa nyara Bob Njagi yuko hai – Rais wa wanasheria
  2. Stoltenberg: Kadiri NATO inavyoipa Ukraine silaha, ndivyo fursa ya kupatikana amani inavyoongezekaStoltenbergChanzo cha picha,EPAKatibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, katika hotuba yake ya kuaga kabla ya kuondoka katika wadhifa wake, alisema kuwa kupatikana kwa amani nchini Ukraine kimsingi kunategemea kiasi cha silaha zinazotolewa kwa Kiev.Stoltenberg pia alibainisha kuwa mazungumzo ya amani yatalazimika kufanywa kwa ushiriki wa Urusi, na alionesha imani kuwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano huo.” Nguvu za kijeshi ni sharti la mazungumzo,” Stoltenberg alisema. “Lazima tuzungumze na majirani zetu, bila kujali hilo linaweza kuwa gumu kiasi gani. Lakini mazungumzo yanafanya kazi pale tu yanapoungwa mkono na ulinzi mkali. Hilo linaonekana wazi katika kesi ya Ukraine.”Wakati huohuo, nguvu za kijeshi zina mapungufu yake, ambayo inaonekana wazi katika mfano wa Afghanistan, aliongeza. “Kwa kuipa Ukraine silaha zaidi, tunaweza kumfanya Putin atambue kwamba hawezi kupata anachotaka kwa nguvu, na kuifanya iwe ya gharama kubwa sana kiasi kwamba atalazimika kukiri kwamba Ukraine ina haki ya kidemokrasia ya kubaki kuwa nchi huru ya kidemokrasia,” aliendelea.”Kitendawili ni kwamba kadiri tunavyoweza kusambaza silaha kwa Ukraine, ndivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba tutaweza kufikia amani na kumaliza vita. Na jinsi msaada wetu wa kijeshi wa muda mrefu unavyotegemewa, ndivyo vita vitaisha haraka. ” Kwa mujibu wa Katibu Mkuu anayemaliza muda wake wa muungano huo, makubaliano yoyote ya baadaye lazima yaungwe mkono na uungaji mkono mkubwa wa kijeshi kwa Ukraine na dhamana ya usalama inayotegemewa ili kuhakikisha amani ya kudumu.Stoltenberg pia alibainisha kuwa hakuwezi kuwa na usalama endelevu katika Ulaya bila Ukraine imara, na hakuwezi kuwa na usalama wa kudumu kwa Ukraine bila uanachama wake katika NATO. “Mlango wa NATO uko wazi,” alisema. “Na Ukraine itajiunga.”Unaweza kusoma;Ukraine itajiunga lini na muungano wa kijeshi wa NATO?

Israel yasema imepiga mitambo 100 ya makombora ya Hezbollah nchini Lebanon

Jet ya Israel

Israel inasema ndege zake za kivita zimeshambulia zaidi ya mitambo 100 ya kurushia roketi za Hezbollah na “maeneo mengine ya kigaidi” ikiwa ni pamoja na kituo cha kuhifadhi silaha kusini mwa Lebanon.

Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) vilisema virusha risasi viko tayari kurushwa dhidi ya Israel.

Haikuweza kufahamika mara moja iwapo kulikuwa na majeruhi.

Shirika la Habari la Taifa la Lebanon limesema kuwa Israel ilifanya mashambulizi 52 kusini mwa nchi hiyo siku ya Alhamisi jioni, na kwamba Lebanon pia ilianzisha mashambulizi katika maeneo ya kijeshi kaskazini mwa Israel.

Hapo awali, kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah alisema milipuko mibaya mapema wiki “ilivuka mistari yote “, akiishutumu Israel kwa kile alichosema kuwa kiliwakilisha tangazo la vita.

Israel haijasema kama ilihusika na mashambulizi hayo, ambayo yalishuhudia vifaa vya mawasiliano kulipuka kwa wakati mmoja nchini kote siku ya Jumanne na Jumatano, na ambayo mamlaka ya Lebanon ilisema iliua watu 37 na kujeruhi 3,000.

Lakini Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant amesema Israel inaanzisha “awamu mpya ya vita”, ikizingatia zaidi juhudi zake kaskazini.

Zaidi ya watu 70,000 waliojitolea kuipigania Urusi wafa Ukraine

Baadhi ya familia hazitoi hadharani maelezo ya vifo vya jamaa zao

Zaidi ya watu 70,000 wanaopigana katika jeshi la Urusi sasa wamefariki nchini Ukraine, kulingana na data iliyochambuliwa na BBC.

Na kwa mara ya kwanza, watu wa kujitolea raia ambao walijiunga na vikosi vya jeshi baada ya kuanza kwa vita, sasa wanaunda idadi kubwa zaidi ya watu waliouawa kwenye uwanja wa vita tangu uvamizi kamili wa Urusi uanze mnamo 2022.

Kila siku, majina ya waliouawa nchini Ukraine, kumbukumbu zao na picha kutoka kwa mazishi yao huchapishwa kote Urusi kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.

BBC Kirusi na tovuti huru ya Mediazona wamekusanya majina haya, pamoja na majina kutoka vyanzo vingine vya wazi, ikiwa ni pamoja na ripoti rasmi.

Tulikagua kufahamu taarifa hiyo ilikuwa imetolewa na mamlaka au jamaa za marehemu na kwamba walikuwa wametambuliwa kuwa walikufa katika vita.

Makaburi mapya pia yamesaidia kutoa majina ya wanajeshi waliouawa nchini Ukraine, haya huwa yana alama za bendera na shada za maua zinazotumwa na wizara ya ulinzi.

Tumetambua majina ya wanajeshi 70,112 wa Urusi waliouawa nchini Ukraine, lakini idadi halisi inaaminika kuwa kubwa zaidi.

Baadhi ya familia hazitoi hadharani maelezo ya vifo vya jamaa zao na uchanganuzi wetu haujumuishi majina ambayo hatukuweza kukagua, au vifo vya wanamgambo katika Donetsk inayokaliwa na Urusi na Luhansk mashariki mwa Ukraine.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment