Jeshi la Israeli limerusha mabomu Kusini mwa Lebanon, baada ya mashambulio kutokea kwenye vifaa vya mawasilino vilivyokuwa vinatumiwa na kundi la Hezbollah, na kusababisha maafa na majeruhi.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Milipuko imesikika hadi katika jiji kuu Beirut, huku vyombo vya habari nchini Lebanon, vikiripoti kuwa ndege za kijeshi za Israeli zimeonekana zikipaa kwenye angaa la nchi yao katika maeneo ya mipaka.
Hatua hii ya jeshi la Israeli inakuja, baada ya Israeli kusema kuwa, inapambana na Hezbollah, kama inavyofanya dhidi ya Hamas kwenye ukanda wa Gaza.
Mbali na kilichoripotiwa kwenye mpaka wa Lebanon, jeshi la Israeli limeendelea kurusha mabomu kwenye ukanda wa Gaza, baada ya watu sita kuuawa kwenye nyumba moja.

Haya yanajiri saa chache tu, baada ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa kura nyingi, kupitisha azimio la kuitaka Israeli kumaliza vita kwenye ukanda wa Gaza na kuondoka kwenye ardhi ya Wapalaestina.
Katika hatua nyingine, vyombo vya Habari nchini Israeli vimeripoti kuwa, nchi hiyo imependekeza mkataba mpya, ili kuachiwa kwa mateka, mapendekezo ambayo yamewasilishwa kwa Marekani ambao ni wasuluhishi wakuu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.