Gabon : Ali Bongo Ondimba amethibitisha kuachana kabisa na siasa

Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo Ondimba, aliyeondolewa madarakani na jeshi mwaka uliopita, amesema anaachana na siasa kabisa na kutaka kuachiwa huru kwa mkewe na mtoto wake wa kiume.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bongo ametoa kauli hii baada ya kuongoza nchi hiyo ya Afrika ya Kati kwa miaka 14, kabla ya wanajeshi kuchukua madaraka mwezi Agosti mwaka uliopita, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.
Bongo ametoa kauli hii baada ya kuongoza nchi hiyo ya Afrika ya Kati kwa miaka 14, kabla ya wanajeshi kuchukua madaraka mwezi Agosti mwaka uliopita, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais. AFP – LUDOVIC MARIN

Bongo ametoa kauli hii baada ya kuongoza nchi hiyo ya Afrika ya Kati kwa miaka 14, kabla ya wanajeshi kuchukua madaraka mwezi Agosti mwaka uliopita, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Kiongozi huyo wa zamani wa Gabon, amesema mbali na kuachana na siasa, ameongeza kuwa yeye sio mtu hatari kwa usalama na umoja wa nchi hiyo, licha ya kuzuiwa kutembelea kwa uhuru.

Baada ya kuondolewa madarakani, Bongo amekuwa akiishi katika makaazi yake binafsi jijini Libreville, huku mkewe Sylvia, mwenye umri wa miaka 61 na Noureddin, mwenye umri wa miaka 32 wakishikiliwa kwa madai ya wizi wa fedha za umma na kujihusisha na biashara haramu.

Serikali ya sasa chini ya Jenerali Brice Oligui Nguema, inaishtumu familia ya rais huyo wa kumtumia vibaya kiongozi huyo wa zamani ili kunufaika na mali za nchi.
Serikali ya sasa chini ya Jenerali Brice Oligui Nguema, inaishtumu familia ya rais huyo wa kumtumia vibaya kiongozi huyo wa zamani ili kunufaika na mali za nchi. © AFP – WILFRIED MBINAH

Hata hivyo, Bongo amesema mkewe na mtoto wake wa kiume wameshikiliwa kwa muda mrefu na wamepitia mateso makubwa kwa kosa ambalo hawajalitenda.

Serikali ya sasa chini ya Jenerali Brice Oligui Nguema, hata hivyo inaishtumu familia ya rais huyo wa kumtumia vibaya kiongozi huyo wa zamani ili kunufaika na mali za nchi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment