DRC: Makabiliano mazito yaripotiwa kati ya MONUSCO na wanamgambo wa CODECO

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kumeripotiwa mapigano makali kati ya askari wa kulinda amani wa MONUSCO na wanamgambo wa CODECO katikati mwa mji wa Bule, ulioko kilomita 90 kaskazini mwa Bunia, katika eneo la Djugu mkowa wa Ituri Kaskazini mashariki mwa DRC.

Serikali ya DRC imekuwa ikipambana na makundi ya waasi katika maeneo ya kivu kaskazini.
Serikali ya DRC imekuwa ikipambana na makundi ya waasi katika maeneo ya kivu kaskazini. AFP – ALEXIS HUGUET

Kwa mujibu wa wakaazi waliokimbia mapigano hayo kutoka mji huo wa Bule, kilomita takribani tisini kaskazini mwa jiji kuu la mkowa huo wa Ituri, Bunia, mapigano hayo yalianza mapema asubuhi ya Alhamisi Ya Septemba 19 baada ya kikosi cha Monusco kuwazuia wanamgambo hawa wa CODECO waliokuwa wakiwashambulia raia katika kambi za watu waliohamishwa za Lala na uwanda wa Savo,

Inadaiwa Wapiganaji hao wa Codeco walimuuwa mwanakijiji ambaye alikuwa akienda mashambani huko Ngle. Maafisa wa Kikosi cha Umoja wa mataifa wamebainisha kupitia tovuti yao.

Wanajeshi wa MONUSCO wamekuwa wakisaidiana na wanajeshi wa DRC katika vita vyake dhidi tya makundi ya waasi mashariki mwa taifa hilo.
Wanajeshi wa MONUSCO wamekuwa wakisaidiana na wanajeshi wa DRC katika vita vyake dhidi tya makundi ya waasi mashariki mwa taifa hilo. AFP – ALEXIS HUGUET

Mashuhuda wanasema tangu Alhamisi asubuhi, milio ya risasi za rashasha na silaha nzito na pia nyepesi imesikika katika eneo hilo, na hivyo kulemaza shughuli zote za kawaida.

Hali sasa ni tulivu baada ya jeshi la Congo FARDC likishirikiana na wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani wakiimarisha usalama katika eneo hilo.

Kusambaza :

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment