Iran yaituhumu Israeli kwa milipuko ya vifaa vya mawasiliano vya Hezbollah

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore

Iran imeituhumu Israeli kwa kile inachosema imetekeleza mauaji ya watu wengi baada ya vifaa vya mawasiliano ya wapiganaji wa Hezbollah wanaouungwa mkono na Tehran nchini Lebanon kulipuka.

Miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye tukio hilo la siku ya Jumanne ni balozi wa Iran nchini Lebanon Mojtaba Amani.
Miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye tukio hilo la siku ya Jumanne ni balozi wa Iran nchini Lebanon Mojtaba Amani. © Aziz Taher / REUTERS

Watu tisa wamethibitisha kuuawa kwenye milipuko hiyo wakati wengine zaidi ya Elfu tatu wakiwa wamejeruhiwa.

Miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye tukio hilo la siku ya Jumanne ni balozi wa Iran nchini Lebanon Mojtaba Amani, Vyombo vya habari vya Iran vikiripoti kwamba balozi huyo alijeruhiwa kwenye mkono na usoni.

Karibia watu wengine 2,800 waliripotiwa kujeruhiwa kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Lebanon.
Karibia watu wengine 2,800 waliripotiwa kujeruhiwa kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Lebanon. REUTERS – Mohamed Azakir

Televisheni inayomilikiwa na serikali ya Iran nayo imeripoti kwamba Amani alipata majeraha madogo.

Nalo shirika la Hilali Nyekundu la Iran limethibitisha kuwapeleka maofisa wa uookoaji na madaktari wa upasuaji kwenda nchini Lebanon kuwasaidia waliojeruhiwa.

Watu wakiwa karibu na gari la kuwabeba wagonjwa baada ya vifaa vya mawasiliano vya wapiganaji wa Hezbollah kulipuka nchini Lebanon (Photo by Anwar AMRO / AFP)
Watu wakiwa karibu na gari la kuwabeba wagonjwa baada ya vifaa vya mawasiliano vya wapiganaji wa Hezbollah kulipuka nchini Lebanon (Photo by Anwar AMRO / AFP) AFP – ANWAR AMRO

Hadi tukichapisha taarifa hii, Israeli haikuwa imezungumzia kuhusiana na milipuko hiyo ambayo ilisababisha vifo vya watu tisa akiwemo mtoto wa miaka 10, binti wa mwanachama wa Hezbollah.

Karibia watu wengine 2,800 waliripotiwa kujeruhiwa kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Lebanon.

Milipuko imetokea saa chache kupita tangu Israeli itangaze kwamba ilikuwa inapanua vita ambavyo vilianzishwa na shambulio la Hamas na tarehe 7 ya mwezi Oktoba.

Kwa mujibu wa Israeli, upanuzi wa vita hivyo ungehusisha wapiganaji wa Hezbollah ambao ni washirika wa Hamas kwenye mpaka wa Israeli na Lebanon.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment