Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Muungano wa Kimataifa wa kutoa chanjo Gavi, umeingia kwenye makubliano na kampuni ya kutengeza dawa ya Bavarian Nordic yenye makao yake nchini Denmark, ili kutoa chanjo 500,000 ya Mpox kwa ajili ya mataifa ya Afrika.

Tangazo hili linakuja, baada ya wiki iliyopita, Shirika la afya duniani WHO kutoa idhini kwa matumizi ya chanjo aina ya MVA-BN, kutumika dhidi ya ugonjwa wa Mpox.
Chanjo hizo zinatarajiwa kuwasili kwenye mataifa mbalimbali ya Afrika yaliyoathirika kufikia mwisho wa mwaka huu.

Aidha, muungano huo umesema utatoa Dola Milioni 9.5 kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuisaidia kupambana na Mpox kwa sababu ndio nchi iliyoathiriwa zaidi barani Afrika, huku mataifa ya Sweden na Thailand, yakiripoti kisa kimoja.
Maambukizo ya Mpox yameendelea kuripotiwa katika mataifa mbalimbali ikiwemo mataifa ya Afrika Magharibi kama Nigeria na Morocco iliyoripoti kisa cha kwanza hivi karibuni, sawa na mataifa jirani ya DRC kama Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.
Mwezi uliopita WHO ilitangaza Mpox kuwa janga la dharura la Kimataifa, baada ya maambukizo kuongezeka nchini DRC na kuanza kusambaa katika mataifa mengine.
Tangu mwezi Januari mwaka huu, watu zaidi ya Elfu 22 wameambukizwa na wengine 700 wamepoteza maisha baada ya kuambukizwa virusi vya Mpox vinavyotoka kwa nyani.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.