Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika ripoti yake, linasema wanajihadi nchini Burkina Faso wameendeleza mashambulio yao na sasa wanawalenga raia wa kawaida.
Human Rights Watch inasema, sababu kubwa ya wanajihadi hao kuwashambulia raia wa kawaida ni kwa sababu raia hao wanakataa kuugana nao.
Sababu nyingine iliyotolewa na Shirika hilo ni kuwa, raia wa kawaida, wanadaiwa na wanajihadi hao kuwa wanashirikiana na wanajeshi wa serikali.
Raia wakawaida, wapatao 128 wameuawa baada ya kushambuliwa kwenye matukio saba yaliyosababishwa na watu wenye silaha, tangu mwezi Februari mwaka huu, vitendo ambavyo Human Rights Watch inasema ni uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.

Aidha, ripoti ya Human Rights Watch, inaeleza kuwa, watu wenye silaha wamekuwa wakivamia vijiji na Makanisa na kuwauwa watu, huku watu wenye ulemavu pia wakilengwa.
Tangu mwaka 2016 wakati Burkina Faso ilipoanza kukabiliwa na utovu wa usalama kutoka kwa makundi ya kigaidi, Shirika la Kimataifa linalokusanya takwimu kuhusu vita, inasema watu Elfu 26 wamepoteza maisha, ikiwemo wanajeshi na raia wa kawaida.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.