Watu wana changamoto ni ile hawapendi kusema.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Sio kila ambaye hakusaidii ni kwamba HATAKI KUFANYA HIVYO.
Kuna wakati unaweza kumuona mtu ana CHEO, PESA au NAFASI na hakusaidii Kama ulivyodhania.
Usimkasirikie, ingawa kuna wengine ndio tabia yao ya kutopenda kusaidia watu.
Ila kuna wakati kunakuwa na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wake.


Kuna nyakati ambazo mtu unayemtarajia akusaidie na yeye yuko kwenye changamoto kubwa Ila anashindwa kukuambia.

Yaani, wakati wewe unamuona ana nafasi na MAMLAKA kubwa sana, kumbe anapitia vita kubwa sana na yuko kwenye hali ngumu.
Wapo wengine pia, kutokana na kuwa na taarifa za ndani sana huwa wanaona sio muda sahihi kwa wao kukuweka mahali fulani.


Wanasubiria muda sahihi au nafasi nzuri zaidi.
Kwa vyovyote vile, mwanadamu ni daraja la kutumiwa na Mungu kukusogeza mahali.
Akishindwa kufanya USIMCHUKIE, bado MUNGU anao uwezo wa kutumia watu wengine.
Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment