Marekani yakamilisha mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger

Jeshi la Marekani hapo jana limetangaza kukamilisha kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini Niger, miezi michache kupita tangu utawala wa kijeshi wa Niamey usitishe ushirikiano wa kijeshi na Washington na kuagiza vikosi vyake kuondoka.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Marekani imekuwa ikiwaondoa wanajeshi wake kwa awamu tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi yaliomuondoa rais Bazoum Madarakani.
Marekani imekuwa ikiwaondoa wanajeshi wake kwa awamu tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi yaliomuondoa rais Bazoum Madarakani. AP – Carley Petesch

Marekani ilikuwa na wanajeshi elfu moja nchini Niger, ambao wamekuwa sehemu ya kikosi cha kupambana na wanajihadi katika ukanda wa Sahel lakini pia kambi ya operesheni za ndege zisizo na rubani.

Kamandi ya kijeshi ya Marekani barani Afrika, AFRICOM, imesema shughuli hiyo imemalizika salama na vikosi ikisifu ushirikiano wa awali uliowezesha kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Niger katika kukabiliana na wanajihadi.

Tangu kupinduliwa kwa rais Mohamed Bazoum, utawala wa kijeshi  chini ya uongozi  wa jenerali  Abdourahmane Tchiani,umekuwa na uhusiano baridi na nchi za magharibi, ikiwemo Mkoloni wake wa zamani Ufaransa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment