Jeshi nchini Mali linasema limedhibiti hali mjini Bamako, mamlaka ikieleza kwamba imefanikiwa kutibua jaribio la watu wenye silaha kuvamia kambi ya jeshi.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Watu wenye silaha walitekeleza shambulio mapema Jumanne dhidi ya kambi ya jeshi katika mji mkuu wa Bamako ambapo milio ya risasi na mlipuko ilisikika.
Watu walioshuhudia tukio hilo akiwemo mwanahabari wa AFP, wanasema hali hiyo ilipelekea kufungwa kwa uwanja wa ndege.
Polisi waliozungumza na AFP wamesema watu hao wenye silaha bado hawajatambuliwa.

Mali imekuwa chini ya utawala wa jeshi tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka wa 2020 na 2021.
Makundi yenye silaha yamekuwa yakitatiza usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi wakiwemo watu wanaotaka kujitenga sawa na wale wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda na Islamic State, wakionekana kulenga hata mji mkuu.
Baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali, mataifa jirani kama vile Burkina Faso na Niger nayo pia yameshuhudia mapinduzi.
Chini ya uongozi wake mkuu wa jeshi Kanali Assimi Goita, Mali ilivunja uhusiano wake na washirika wake wa bara Ulaya ikiwemo mkoloni wake wa zamani Ufaransa.
Mali imeonekana kugeukia upande wa Urusi na wapiganaji wa Wagner kwa msaada wa kijeshi baada ya kukatiza uhusiano wake na Ufaransa
Viongozi wa kijeshi wameahidi kudhibiti tena maeneo yanayokaliwa na makundi yenye silaha kwenye taifa hilo na kurejesha usalama.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.