Nigeria: Wafungwa 270 hawafahamiki waliko baada ya kutoroka jela

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Nigeria inasema, wafungwa 270 hawafahamiki waliko, baada ya kutoroka jela katika mji wa Maiduguri ulioshuhudia mafuriko makubwa na kuharibu miundo mbinu likiwemo gereza hilo.

Hii ndio mara ya kwanza kwa serikali nchini Nigeria, kukiri kutoroka kwa wafungwa baada ya mafuriko makubwa yaliyosabibishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha, kuangusha kuta za jela  ambayo wafungwa hao wamekuwa wamezuiwa.
Hii ndio mara ya kwanza kwa serikali nchini Nigeria, kukiri kutoroka kwa wafungwa baada ya mafuriko makubwa yaliyosabibishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha, kuangusha kuta za jela  ambayo wafungwa hao wamekuwa wamezuiwa. © AUDU MARTE / AFP

Hata hivyo, maafisa wa Magereza wamesema, wafungwa saba wamerejea jela, baada ya kutoroka wiki iliyopita.

Hii ndio mara ya kwanza kwa serikali nchini Nigeria, kukiri kutoroka kwa wafungwa baada ya mafuriko makubwa yaliyosabibishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha, kuangusha kuta za jela  ambayo wafungwa hao wamekuwa wamezuiwa.

Mafuriko hayo makubwa, yamesababisha maafa ya watu 30 katika mji huo unaopatikana katika jimbo la Borno, na kuwaacha maelfu bila makaazi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.

Aidha, kuvunjika kwa kingo za bwawa la  Alau, kulisababisha wanyama wakali kama mamba na nyoka kusombwa na maji hadi katika makaazi ya watu, baada ya mafuriko kuharibu mbunga ya wanyama inayomilikiwa na serikali.

Rais Bola Tinubu, siku ya Jumatatu, anatembelea mji wa Maiduguri kujionea madhara makubwa yaliyosababishwa na mafuriko hayo makubwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment