Usiogope ewe Shujaa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Yapo aina ya MAAMUZI ambayo YATAUMIZA MOYO wako kwa MUDA MFUPI Ila yatakupa FURAHA na UHURU wa KUDUMU.

Kuna watu wengi sana kwa KUOGOPA MAUMIVU, wameishia kughairisha kufanya MAAMUZI MUHIMU YA MAISHA YAO.

Kuna watu wameshachelewa kufanya maamuzi kuhusu kazi, mahusiano au biashara zao na Matokeo Yake mambo yanazidi KUHARIBIKA.

Ni muhimu kujua kuwa, kuna aina fulani ya MAUMIVU ni ya LAZIMA. Yaani, hauwezi kusema, kuna siku itafika SITAYAHISI Hapo ndio nifanye maamuzi, HAIWEZEKANI.

Haujui kuna aina ya MAUMIVU ni sehemu ya UPONYAJI? Yaani, ili upone lazima ukubali kuyasikia MAUMIVU. Ukijihurumia SANA, unazidi KUJICHELEWESHA.

Amua kuyafanya LEO, uanze mchakato wa KUPONA MAPEMA ili uendelee na maisha. Usiendelee KUGHAIRISHA kila SIKU.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment