Usichukue sifa za watu wengine.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye maisha utakutana na watu ambao huwa wanapenda KUCHUKUA SIFA za watu wengine.

Yaani, wao hawafanyi, ila wanataka sifa zote ziwaendee wao.

Hawa utakutana nao kwenye ofisi, Michezo, biashara, Siasa n.k

Kuna watu wengi sana ambao waliwahi kuwa na mawazo mazuri ila wakashirikisha mtu.

Kisha huyo mtu akalichukua na kulifanya lake.

Kwa sababu pengine ya ukubwa wake wa nafasi, Pesa au Umaarufu; akajimilikisha.

Mwenye wazo wa kwanza akabakia ni “ndugu Mtazamaji”.

Nimewahi kukutana na watu wengi wenye maumivu makali ya kuibiwa mawazo au sifa walizostahili.

Zingatia jambo la kwanza, jifunze kwenye kila kinachokutokea.

Tafuta kujua namna ya kuhusiana na watu, usiamini watu kirahisi kwenye kila kitu.

Pili, bakiza “password” ya wazo lako.

Yaani, bakiza kitu ambacho hata wakianza kulitekeleza kuna mahali watakuhitaji.

Hata kama ulishaumizwa kwa kuibiwa wazo lako, usiache kupambania mawazo yako Mapya.

Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment