Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Usiache kwa sababu UMEFELI…
Kwenye maisha yangu nimewahi KUFELI kwenye mambo mengi sana.
Nimewahi kufeli darasani na kuwa mtu wa 3 kutoka mwishoni.
Nimewahi Kufeli kwenye biashara kadhaa na nikapoteza mtaji.
Nimewahi kugombea nafasi kadhaa za Uongozi na nikafeli.
Nimeshawahi kuandaa semina na watu wakaja wachache…
…ikabidi nikope Pesa za kulipia gharama.
Yaani, katika chochote ambacho unakiona kwangu ni mafanikio…
…nyuma Yake kuna KUFELI kwangu ambako haujakuona.
Bila kujali mtu na uwezo mkubwa kiasi gani, kufeli njiani ni sehemu ya safari ya maisha.
Usiogope kufeli wala usikate tamaa kwa sababu umefeli.
Henry Ford aliwahi kusema…
“Failure is simply the opportunity to begin again, this time more intelligently”.
Akimaanisha, kufeli ni fursa nyingine unayopewa ili kuanza upya ukiwa na maarifa makubwa zaidi.
Sahau ULIVYOFELI, anza kujipanga upya na kuchukua hatua KUPAMBANIA NDOTO YAKO.
Kama umeipenda makala hii…
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.