Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mchezaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala anawaniwa na Liverpool, Manchester United waimarisha juhudi za kumsajili Xavi Simons kutoka Paris St-Germain, huku West Ham wakimtaka Joel Matip.
Liverpool wamepiga hatua katika juhudi za kumnunua kiungo wa Bayern Munich Jamal Musiala, 21, huku klabu za Manchester City, Real Madrid na Paris St-Germain zikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Caughtoffside)
Manchester United wana matumaini ya kumnunua winga wa Paris St-Germain Xavi Simons baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 21 – ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo RB Leipzig – kusema haoni mustakabali wa klabu hiyo ya Ligue 1. (TeamTalk)
Manchester United na Arsenal wamesitisha mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru, baada ya kushindwa kufikia mshahara ya pauni 220,000 kwa wiki unaoitishwa na mchezaji huyo. (GiveMeSport)

Manchester United iliwaorodhesha mshambuliaji wa Lille raia wa Canada Jonathan David, 24, na mshambuliaji wa Al-Ahli na Uingereza Ivan Toney, 28, kama mbadala wa Joshua Zirkzee wakimkosa Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Bologna. (ESPN)
Inter Milan wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Aston Villa Muingereza Jacob Ramsey, 23. (Caughtoffside)
Mshambulizi wa Chelsea na Ivory Coast David Datro Fofana amefikia mkataba wa mkopo na klabu ya Uturuki Goztepe SK baada ya jaribio la mchezaji huyo wa miaka 21 kuhamia AEK Athens kutibuka. (Fabrizio Romano)
West Ham wana nia ya kumsajili mlinzi wa zamani wa Liverpool Joel Matip, 33, kwa uhamisho wa bure kwani mlinzi huyo wa Cameroon mzaliwa wa Ujerumani bado hajapata klabu. (Ruhr24 – kwa Kijerumani)
Beki wa zamani wa Uingereza na Chelsea Ashley Cole anatarajiwa kuacha nafasi yake ya ukocha katika klabu ya Birmingham City na kujiunga na Shirikisho la Soka na kufanya kazi na mkufunzi wa muda wa Uingereza Lee Carsley. (Athletic – usajili unahitajika)
Beki wa Chelsea Muingereza Ben Chilwell anatumai kujumuishwa katika kikosi cha wachezaji 25 cha klabu hiyo kinachoshiriki Ligi ya Premia, kwakuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatarajiwi kuhamia Uturuki kwa mkopo. (Telegraph – usajili unahitajika)
Arsenal na Chelsea zinatarajiwa kumjumuisha mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kwenye orodha yao ya wachezaji watakaowanunua dirisha la usajili la majira ya joto litakapofunguliwa. (Football Insider)

Junior Firpo anataka kusaini kandarasi mpya huko Leeds lakini beki huyo wa Jamhuri ya Dominica mwenye umri wa miaka 28 yuko tayari kurejea La Liga iwapo makubaliano hayatafikiwa, huku Real Betis wakiwa na nia ya kumsajili. (Team Talk)
Beki wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos, 38, anatazamia kuhamia Ligi Kuu ya Soka baada ya jaribio la Mhispania huyo kuhamia Botafogo ya Brazil kugonga mwamba. (Goal)
Wakala wa winga wa Athletic Bilbao Nico Williams anasema Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 22 alipuuza kuhamia Barcelona kwa sababu alitaka kusalia na Klabu ya Basque kwa mwaka mwingine. (AS – kwa Kihispania)
Wamiliki wa AC Milan hawajaridhishwa na mwenendo wa mshambuliaji wa zamani wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic ,42, kama mshauri mkuu wa klabu hiyo. (La Repubblica – kwa Kiitaliano)
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.