Mivutano yazidi kushuhudiwa ndanI ya chama cha rais Tshisekedi wa DRC

Chama tawala nchini DRC, Union for Democracy and Social Progress (UDPS), kinachoongozwa na Rais Félix Tshisekedi, kinaendelea kushuhudia mivutano na mpasuko zaidi wa kimadaraka tangu Tshisekedi aingie madarakani.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa DRC,  Félix Tshisekedi.
Rais wa DRC, Félix Tshisekedi. AFP – CHRISTOPHE ENA

Chanzo cha Mgogoro unaoendelea na unaotishia kumvuruga Rais katika juhudi za kuleta utulivu ndani ya chama hicho ni Katibu Mkuu Augustin Kabuya, ambaye baadhi ya  wanaharakati wanataka aachie ngazi ili kukipanga upya chama hicho, vita za ndani ya chama sasa zikiwa dhahiri.

Mzozo ulianza mwaka 2019, ambapo Tshisekedi, mwenyekiti wa chama hicho wakati huo, alitakiwa kukabidhi madaraka kwa Jean-Marc Kabund na Augustin Kabuya ambao walipewa mamlaka ya kukalia, kwa muda, nyadhifa za mwenyekiti na katibu mkuu mtawalia.

Augustin Kabuya, chef du parti présidentiel et informateur à l'Assemblée nationale de RDC, lors d'une conférence de presse à Kinshasa, le 15 février 2024.
Augustin Kabuya, chef du parti présidentiel et informateur à l’Assemblée nationale de RDC, lors d’une conférence de presse à Kinshasa, le 15 février 2024. © Pascal Mulegwa/RFI

Hata hivyo baada ya muda, Kabunda aligeuka mpinzani wa Tshisekedi na kutupwa jela, huku Kabuya akisalia akimuheshimu tu rais Thisekedi ambaye hawezi tena kufanya maamuzi rasmi ya chama.

Vita ndani ya chama imefikia pabaya kiasi hata Rais Tshisekedi kumtumia mama yake, Marthe Kasalu kujaribu kuzipatanisha pande zinazozozana hata hivyo bila mafanikio.

Hata hivyo, Kabuya ni kama ametupwa nje baada ya makada wa chama kumchagua Deogratias Bizibu kuchukua nafasi yake.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment